2013-07-24 07:52:48

Maadhimisho ya Siku ya Vijana Dunani yajenge na kuimarisha imani, upendo na mshikamano wa kidugu!


Kardinali Tarcisio Bertone, Katibu mkuu wa Vatican, katika Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani, ametoa medali ya kumbu kumbu ya hija ya kwanza ya kichungaji kufanywa na Baba Mtakatifu Francisko, tukio ambalo limehudhuriwa na viongozi wa Kanisa, Serikali na umati mkubwa wa vijana.

Kardinali Bertone, amewapongeza wale wote walioshughulika kuandaa medali hizi kwa ajili ya kumbu kumbu ya tukio hili la kiimani, ambalo limewakusanya vijana kutoka sehemu mbali mbali za dunia. Medali inamwonesha jinsi ambavyo Baba Mtakatifu Francisko alivyo karibu zaidi na watu. Medali hizi ziwasaidie waamini na wote wenye mapenzi mema kufurahia zawadi ya imani, kwa kushirikishina mwanga wa upendo, mshikamano na udugu, kama alivyosema Baba Mtakatifu Francisko katika hotuba yake alipowasili nchini Brazil.

Kardinali Bertone, anawachangamotisha wadau mbali mbali kusikiliza kwa makini yale yatakayozungumzwa wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani ili hatimaye, waweze kuyamwilisha katika uhalisia wa maisha yao.







All the contents on this site are copyrighted ©.