2013-07-22 12:05:44

Salam na matashi mema kutoka kwa Papa Francisko kwa wakuu mbali mbali wa nchi


Baba Mtakatifu Francisko wakati wa safari yake ya kichungaji kuelekea Rio de Janeiro, Brazil amewaandikia ujumbe marais na wakuu wa nchi mbali mbali ambamo atapita wakati wa safari yake amewaombea: baraka, amani na utulivu. Katika salam zake kwa Rais Giorgio Napolitano wa Italia, Baba Mtakatifu anasema, anakwenda Brazil ili kukutana na vijana kutoka sehemu mbali mbali za dunia, ili aweze kuwaimarisha wawe ni mashahidi wa upendo na wajenzi wa amani.

Baadhi ya wakuu wa nchi walioandikiwa ujumbe na Baba Mtakatifu Francisko ni: Italia, Algeria, Mauritania na Senegal.







All the contents on this site are copyrighted ©.