Papa Francisko na Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XV1 pamoja waombea Mkutano wa 28
wa Vijana Rio.
Ijumaa zikiwa zimebaki siku tatu kabla ya kufanya ziara yake ya kwanza ya Kitume
ya Kimataifa, kutembelea Rio de Janeiro Brazil, Papa Francisko, kwa moyo wa upendo
na uungwana namshikamano wa karibu na mtagulizi wake, alikwenda kumtembelea Mstaafu,
Papa Benedikto XV1, katika monesteri ya Vatican, kumwomba aongozane nae kiroho katika
ziara hii aliyoiitisha yeye Papa Ratzinger. Maelfu ya vijana wanaendelea kukusanyika
Rio de Janeiro, kwa ajili ya maadhimisho 28 ya Siku ya Vijana ya Dunia, na Papa Francisko
atakwenda kuungana nao siku Jumatatu hii 22 Julai 2013. Ijumaa, Papa Benedict XVI
na Francisko walipokutana walipata muda wa nusu saa wa kusali pamoja, wakiombea tukio
hili la WYD na walishirikishana mawazo juu ya tukio hili. Papa Francisko pamoja nae
alikuwa na medali maalum aliyoiandaa kama kumbukumbu ya safari na pia alikuwa na kijitabu
kidogo , vitu alivyo mzawadia Mstaafu Papa Benedict XVI, ambaye alisema kwa hakika
vitamkumbusha kutolea sala zake na kuwa nae karibu kiroho wakati wote na hasa katika
siku zote za tukio hili, linalo mkumbusha maadhmisho aliyoyashiriki huko Cologne,
Sydney na Madrid. Papa Francisko, Jumatatu 22 Julai 2013, majira ya saa tatu, ataanza
safari ya kuelekea Rio de Janeiro, ambako kwa muda wa wiki zima ataungana na Vijana
kwa ajili ya Maadhimisho ya 28 ya Siku ya Vijana ya Dunia. Papa anakwenda kukutana
na vijana kwa lengo la kuwaimarisha kiroho, kama inavyotaja madambiu kwa adhimisho
– “Nendeni mkawafanye wote kuwa wanafunzi wangu”. Hivyo ni maadhimisho ya kuitangza
Injili ya Upendo wa Yesu wa kuokoa. Katika sherehe hizi, akti ya mambo mengine Papa
ataongoza Ibada za misa, njia ya Msalaba na Mkesha wa sala.