2013-07-20 10:02:23

Baba mtakatifu mstaafu Benedikto XVI amesema, atamsindikiza Papa Francisko wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Vijana kwa Sala!


Papa Francisko, Ijumaa jioni kama sehemu ya maandalizi ya hija yake ya kichungaji kwa ajili ya Maadhimisho ya Siku ya 28 ya Vija Duniani, inayoadhimishwa huko mjini Rio de Janeiro, amemtembelea Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto wa kumi na sita, ili kumwomba aweze kumsindikiza katika hija hii ya kichungaji kwa njia ya sala. Haya ni maadhimisho yaliyokuwa yamekwishapangwa na Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto wa kumi na sita.

Papa Francisko amemzawadia kitabu cha ratiba elekezi ya Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani, ili pale atakapoona inafaa aweze kufuatilia tukio hili la kiimani, lakini jambo la msingi ni kuwasindikiza kwa sala na sadaka yake. Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto wa kumi na sita, amemhakikishia Papa Francisko kwamba, atawasindikiza kwa sala na kwamba, amemshirikisha mang'amuzi na uzoefu wake katika Maadhimisho ya Siku za Vijana Duniani huko Colony, Sydney na Madrid. Mazungumzo yao yalitanguliwa kwa sala ya pamoja kwenye Kikanisa na baadaye, wakaendelea na mazungumzo.







All the contents on this site are copyrighted ©.