2013-07-20 14:11:18

Amani ni zawadi ya Mungu, hupata nafasi katika moyo unaoridhia kuipokea.


Ijumaa 19 Julai ilikamilika miaka 70, tangu mji wa Roma uliposhambuliwa kwa mabomu wakati wa kipindi cha vita kuu ya Pili ya Dunia, shambulio linalijulikana hapa Italy kama "mabomu ya San Lorenzo".
Papa Francisko akiungana na wakazi wa jiji la Roma, kuikumbuka siku hii ya iliyo kuwa ya huzuni kubwa miaka sabini iliyopita, alisema Amani, zawadi ya Mungu, bado hupata nafasi katika mioyo inayopenda kuipokea.
Amewakumbusha watu wa Roma na taifa la Italia kwa ujumla kwamba, kumbukumbu hii ya mbaya inayojulikana kama "mabomu ya Mtakatifu Lorenzo", kwa kuwa uharibifu mkubwa ulifanyika katika Kanisa kuu la Mtakatifu Lorenzo, miaka sabini iliyopita, kwa wakati huu inakuwa ni fursa ya kutolea sala na maombi kwa ajili ya kafara wote wa mabomu hayo. Huu ni wakati wa kutafakari juu ya vita, kuuona utendaji wa kivita kama ni mijeledi. Na haiwezekani kuikumbuka siku hii, bila akili kurejesha kumbukumbu na kumshukuru Papa Pius XII, k uwepo wake , mafundisho yake na utendaji wake wa kibaba, alio uonyesha mara baada ya kupata taarifa za uhalibifu huo wa mabomu, katika maeneo kadhaa ya jiji la Roma.

Papa Francisko amesisitiza katika telegramu aliyomtumia Kardinali Agostino Vallini,Vika wa Jimbo la Roma, siku ya Ijumaa , wakati akiongoza Ibada ya Misa katika Kanisa Kuu la Verano, kwa ajili ya kumbukumbu hii.
Papa Francisko alisema, amani ni zawadi ya Mungu, kwa moyo wenye nafasi,inayotafuta kujenga amani na maridhiano. alieleza hasa kwa kuangalisha katika moyo wa namna hiyo wa Papa Pius XII, ambaye mwaka 1939, alitoa ujumbe wa kusisimua kwa njia ya Redio m akiomba amani na maeelzo kwamba, hakuna kinachopoa kwa kujenga amani, lakini vita inaweza kuyaangamiza yote. Ujumbe huo wa Papa Pacelli ,Ulipelekwa sehemu mbalimbali katika Makanisa yote, Parokia, mahali pa hadhara, katika taasisi za kidini, shule za bweni, ukilenga kutoa faraja kwa uuma wote. Maaskofu, mapadre , na watawa katika mashirika wote walitiwa nguvu na maneno ya Papa Pius XII, na kujitokeza kwenda nje kuhudumia wahitaji, kama msamaria mwema. s
Kwa ajili ya maadhimsho haya , Ijumaa kulifanyika mkutano wa maonyesho yaliyozinduliwa na Mheshimiwa Roma, Ignazio Marino. Kwa hakika ilikuwa ni tarehe 19 Julai 1943, mabomu yaliipo miminwa katika eneo la jiji la Roma na kuua watu 1500 wafu na 4000 kujeruhiwa.ilikuw niwakati wa huzuni kubwa na Papa Pacelli alitoa kilio cha amani.

Kwa wema alioufanya Papa Pacelli wakati wa vita vya dunia Kanisa lilimtaja kuwa Mwenye Heri.







All the contents on this site are copyrighted ©.