Vitendo vya uharamia vilivyokuwa vimeanza kutulia kidogo mara baada ya Jumuiya ya
Kimataifa kulivalia njuga tatizo hili, vimeanza kujitokeza tena huko Afrika Magharibi.
Hivi karibuni Meli iliyokuwa imebeba shehena ya kemikali ilitekwa nyara na
maharamia kutoka Togo, hali ambayo imeanza kutishia usalama wa maisha na bidhaa kwenye
Ghuba ya Afrika Magharibi inayoziunganisha nchi za Nigeria, Togo, Ghana na Pwani ya
Pembe. Hizi ni nchi ambazo zinasafirisha bidhaa nyingi kwenye soko la kimataifa kwa
kupitia mlango wa bahari.
Uharamia umepelekea Makampuni ya Meli kuongeza gharama
za bima, hali ambayo imesababisha watu wengi kutowekeza katika sekta ya usafirishaji
baharini.