2013-07-19 15:02:03

Ajali mbaya ya bus yatokea kwa vijana Mahujaji wa WYD 2013- tokea French Guiyana


Jumatano, huko French Guiyana, ilitokea ajali mbaya ya bus lililokuwa likisafirisha vijana Wafaransa , katika kuianza hija ya kuelekea Rio de Janeiro, kwa lengo la kushiriki katika adhimisho la 28 la Siku ya Vijana ya Dunia WYD. Bus hilo liligongana uso kwa uso na lori na kusababisha binti mmoja kufariki papo hapo na wengine watatu hali zao zinatajwa kuwa mbaya.
Alhamis, Baba Mtakatifu Francisko, mara baada ya kupata habari hii ya kusikitisha, kiroho aliunganika katika mateso na majonzi ya vijana hao na familia zao.
Papa kupitia Katibu wa Vatican Kardinali Tarcisio Bertone, alituma telegram ya rambirambi kwa Askofu wa Cayenne, kwa niaba ya Maaskofu wote wa French Guiyana , ambamo ameonyesha masikitiko yake kwa ajali hiyo. Na ametoa baraka zake za kipapa kwa kafara wote wa ajali, na pia kwa wale waliowasaidia vijana baada ya ajali kutokea, na wote wale walioguswa na msiba huu.
Ajali hiyo ilitokea katika barabara kuu inayounganisha mji wa Saint Laurent du Maroni na mji wa Cayenne, baada ya bus kusafiri umbali wa kilomita 12. Katika bus hilo kulikuwa na wasafiri 23.
Taarifa zinasema, mjini Paris Ufaransa, Alhamis jioni, Kardinali Andre Vingt Trois, wa Jimbo Kuu la Paris, aliongoza Ibada ya Misa katika Parokia ya Mtakatifu Leonè ambako kafara wa ajali wanatokea kwa nia ya kumwombea Marehemu na wote waliodhurika katika ajali hii na familia zao. Vivyo hivyo Askofu wa Cayenne, aliongoza Ibada ya Misa katika Kanisa kuu la Cayenne kwa nia hiyo ya kuwaombea kafara.








All the contents on this site are copyrighted ©.