Katika Maadhimisho ya Mwaka wa Imani uliotangazwa na kuzinduliwa na Baba Mtakatifu
mstaafu Benedikto wa kumi na sita kama sehemu ya Maadhimisho ya Jubilee ya miaka 50
ya Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican na Miaka 20 tangu Katekisimu Mpya ya Kanisa Katoliki
ilipochapishwa; Baba Mtakatifu Francisko anawakumbusha watumiaji wa mitandao ya kijamii
kwamba, imani si zawadi ya mtu binafsi, bali inapaswa kuwashirikisha wengine. Kila
Mkristo ni mtume wa Yesu.