Mali kuingia kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu hapo tarehe 28 Julai 2013, lakini
kampeni zimedorora!
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban Ki-Moon, amewataka wanasiasa nchini Mali
kuhakikisha kwamba, uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika nchini humo hapo tarehe 28
Julai 2013 unakuwa huru na wa haki na kwamba, wanasiasa wakubali pia matokeo.
Jumuiya
ya Kimataifa inaendelea kufuatilia kwa ukaribu mchakato wa uchaguzi mkuu ili kufunga
kipindi cha serikali ya mpito, iliyoingia madarakani kunako mwezi Mei, 2012 baada
ya Serikali iliyokuwa imechaguliwa kihalali kupinduliwa kutoka madarakani.
Wachunguzi
wa mambo wanasema, kwa sasa kampeni bado hazijaanza kushika kasi ya kutosha licha
ya muda kuzidi kuyoyoma kwa kasi. Hii inachangiwa pengine na Mfungo Mtukufu wa Mwezi
Ramadhani, kwani asilimia 90% ya wananchi wa Mali ni waamini wa dini ya Kiislam. Kuna
jumla ya wanasiasa 28 wanaowania kuchaguliwa kuongoza Mali kama Marais.