2013-07-17 10:56:20

Kanisa ladai haki ya afya kwenye mchakato wa Katiba Mpya Ghana!


Baraza la Maaskofu Katoliki Ghana limeiomba Serikali nchini humo kuhakikisha kwamba, inatambua haki ya afya katika mchakato wa kuandika Katiba Mpya ya Ghana. Baraza la Maaskofu Katoliki Ghana limeanzisha kampeni inayolenga kubadilisha Kipengele cha Katiba ya Mwaka 1992 inayozungumzia kuhusu haki za mgonjwa.

Maaskofu wanasema, hapa jambo la msingi ni wananchi kuwa na haki ya afya, ili kutoa fursa sawa kwa kila mwananchi wa Ghana kuweza kupata huduma za afya kama sehemu yake Kikatiba. Kampeni hii inawahusisha Waamini na Watu wote wenye mapenzi mema nchini Ghana. Maaskofu wanakazia umuhimu lishe, afya bora, huduma bora za afya pamoja na kuangalia matatizo na changamoto zinazojitokeza katika sekta ya afya tangu kijijini hadi mijini.

Takwimu za Shirika la Afya Duniani zinazonesha kwamba, nchini Ghana kuna jumla ya watu millioni mbili wenye ulemavu. Hawa wanaunda asilimia 7 hadi 8% ya Idadi ya watu nchini Ghana.







All the contents on this site are copyrighted ©.