2013-07-16 11:14:27

ICC: Rais Uhuru Kenyata na William Ruto kesi yao haiwezi kusikilizwa Kenya!


Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai imetupilia mbali rufaa ya Rais Uhuru Kenyata na Makamu wake wa Rais William Ruto ya kutaka kesi inayowakabili mahakamani hapo, isikilizwe nchini Kenya, baada ya kutuhumiwa kujihusisha na machafuko ya kisiasa yaliyoibuka mara tu baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika kunako mwaka 2007.

Katika machafuko hayo, watu 1200 walipoteza maisha na wengi kulazimika kuyakimbia makazi yao. Mahakama ya Kimataifa ilikuwa inaafiki wazo la kusogeza kesi kwa Jumuiya iliyoathirika, lakini kwa kesi ya Kenya, jambo hili haliwezekani.







All the contents on this site are copyrighted ©.