2013-07-16 11:50:56

China ni mwekezaji mkubwa nchini Angola


China ni kati ya wadau wakuu wa biashara nchini Angola ambayo katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni, biashara kati ya nchi hizi mbili imeongezeka maradufu, kiasi cha kufikia dolla za kimarekani billioni tatu, ambayo ni asilimia 43% ya biashara yote kutoka China.

Taarifa zinaonesha kwamba, Angola imeuza bidhaa zake nchini China na kupata kiasi cha billioni 2.5, ambacho ni asilimia 11% ya bidhaa zote zilizoagizwa na China kutoka Angola. China imewekeza kwa kiasi kikubwa nchini Angola katika sekta ya ujenzi, vifaa vya umeme na nguo kiasi cha kutawala soko la Angola ambalo lina mvuto mkubwa kutoka sehemu mbali mbali za dunia.







All the contents on this site are copyrighted ©.