2013-07-15 09:55:24

Mandela Day, 18 Julai 2013


Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini anasema, katika kumbu kumbu ya Maadhimisho ya Miaka 95 ya kuzaliwa kwa Mzee Nelson Mandela, hapo tarehe 18 Julai 2013, wananchi wa Afrika ya Kusini wataikumbuka kwa namna ya pekee, huku wakiongozwa na kauli mbiu "tenda na changia mabadiliko ili kila siku, iwe ni kumbu kumbu ya Nelson Mandela".

Katika Maadhimisho hayo, Serikali ya Afrika ya Kusini, inatarajiwa kukabidhi makazi mapya kwa wananchi wanaoishi Bethleem na Hermanstad, yaliyoko mjini Pretoria kama kielelezo makini cha Mzee Madiba katika mapambano dhidi ubaguzi wa rangi, uliopelekea mchakato wa ujenzi mpya wa Afrika ya Kusini inayosimikwa katika ukweli, haki na upatanisho.







All the contents on this site are copyrighted ©.