Wakati huu ambapo utandawazi na maendeleo ya sayansi na teknolojia yanatishia ustawi
na maisha ya binadamu, Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa
mitandao ya kijamii anawakumbusha kwamba, kwa Mkristo, maisha si jambo la bahati nasibu!
Bali ni tunda la mwaliko wa upendo kwa mtu binafsi.