Onesheni ushuhuda wa Mwaka wa Imani kwa njia ya matendo!
Katika Maadhimisho ya Mwaka wa Imani uliotangazwa na kuzinduliwa na Baba Mtakatifu
mstaafu Benedikto wa kumi na sita, sanjari na Jubilee ya miaka 50 ya Mtaguso Mkuu
wa Pili wa Vatican na kumbu kumbu ya miaka 20 ya Katekesi Mpya ya Kanisa Katoliki,
Baba Mtakatifu Francisko anawaalika watumiaji wa mitandao ya kijamii, kuhakikisha
kwamba, walau wanafanya tendo la huruma kila siku, kama njia ya kumfahamu Kristo vyema
zaidi.