2013-07-12 08:21:32

Papa Francisko ashiriki kikao cha kwanza cha Tume ye Benki ya Vatican


Kwa mara ya kwanza Tume ya Kipapa ya Benki ya Vatican imefanya kikao chake kwenye Makazi ya Domus Sanctae Marthae yaliyoko mjini vatican na kuhudhuriwa na Baba Mtakatifu Francisko. Kikao hiki kimehudhuriwa pia na viongozi waandamizi wa Benki ya Vatican, IOR.

Katika mkutano huu, Baba Mtakatifu amewatia moyo wajumbe kuendelea na kazi yao kwa umakini mkubwa kwa ajili ya mafao na ustawi wa Kanisa. Mkutano huu umefanyika Jumatano, tarehe 10 Julai 2013.







All the contents on this site are copyrighted ©.