2013-07-12 08:39:32

Jumapili tarehe 14 Julai 2013, Papa kuongoza Sala ya Malaika wa Bwana, Ikulu Ndogo ya Castel Gandolfo


Baba Mtakatifu Francisko, Jumapili tarehe 14 Julai 2013 anatarajiwa kuongoza Sala ya Malaika wa Bwana, akiwa kwenye Ikulu Ndogo ya Castel Gandolfo, nje kidogo ya mji wa Roma. Akiwa Castel Gandolfo, Baba Mtakatifu atatumia fursa hii kukutana na kuzungumza na wafanyakazi wa Ikulu Ndogo ya Castel Gandolfo ambayo hutumika kwa ajili ya mapumziko ya Papa wakati wa Kipindi cha Joto.

Hii itakuwa ni nafasi kwa Baba Mtakatifu kukutana na kuzungumza pia na viongozi wa Kanisa na Serikali wa Mji wa Castel Gandolfo. Hii itakuwa ni mara ya pili kwa Baba Mtakatifu Francisko kutembelea Castel Gandolfo, tangu alipochaguliwa kuliongoza Kanisa kama Khalifa wa Mtakatifu Petro. Mara ya kwanza ni wakati ule alipokwenda kumtembelea na kusali na Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto wa kumi na sita, tukio la kihistoria ambalo limeacha kumbu kumbu katika mioyo ya waamini wengi hapo tarehe 23 Marchi 2013.







All the contents on this site are copyrighted ©.