Mheshimiwa Padre Nkea Fuanya ateuliwa kuwa Askofu Mwandamizi wa Jimbo Katoliki Mamfe,
Cameroon
Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Nkea Fuanya kutoka Jimbo Katoliki
la Buèa, kuwa Askofu Mwandamizi wa Jimbo Katoliki la Mamfe, Cameroon. Hadi kuteuliwa
kwake alikuwa ni Katibu mkuu wa Chuo Kikuu Cha Kikatoliki nchini Cameroon.
Askofu
mteule alizaliwa tarehe 29 Agosti 1965 ambalo kwa wakati huo lilikuwa ni Jimbo kuu
la Bamenda. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapewa Daraja Takatifu
la Upadre kunako tarehe 22 Aprili 1992 kwa ajili ya Jimbo Katoliki la Buèa, Cameroon.
Tangu wakati huo amefanya kazi mbali mbali za kichungaji hadi kunako mwaka 1999 hadi
mwaka 2003 alipokwenda Roma kwa ajili ya masomo ya juu na kujipatia shahada ya uzamivu
kutoka katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana.
Kunako mwaka 2003 hadi mwaka
2007 alikuwa ni Katibu mkuu wa Jimbo. Mwaka 2007 hadi mwaka 2010, akapelekwa kufundisha
na kuwa mlezi, Seminari kuu ya Mtakatifu Thomas D'Aquin iliyoko Bamenda. Kuanzia mwaka
2010 alibahatika kupangia shughuli mbali mbali katika Baraza la Maaskofu Katoliki
Cameroon, Jimbo kuu Bamenda katika masuala ya Sheria za Kanisa na hatimaye, akawa
ni Katibu mkuu wa Chuo Kikuu cha KIkatoliki cha Cameroon.