Kuwa Mkristo haihitaji kufanya mengi , bali ni kuruhusu kufanywa upya na Roho Mtakatifu.
Ni msisitizo wa Papa Francisko wakati wa Ibada ya Misa mapema Jumamosi , ibada aliyo
iongoza katika Kanisa dogo la Mtaktifu Marta la mjini Vatican, ikiw ani ibada yake
ya mwisho kabla ya mapumziko ya kipindi cha majira ya joto Ulaya, baada ya kuwa na
mfululizo wa Ibada zake za asubuhi alizo ziongoza katika kanisa dogo la Mtakatifu
Marta tangu achaguliwe kuwa Papa. Katika Ibada hiyo ya Jumamosi pia alisema , hata
katika maisha ya kanisa, kuna miundo ya kale, bila shaka inayohitaji kufanywa upya
. Miongoni mwa waliohudhuria Ibada hiyo ni pamoja na kundi la Walinzi wa Kipapa,
"The Uswiss Guards ".
Homilia ya Papa ililenga katika somo la Injili juu
ya mfano wa Mvinyo mpya juu ya Mivinyo mingine, na alirejea utajiri wa mafundisho
ya Yesu , juu ya sheria , akisema , Yesu alifanya mambo yote kuwa mapya. Na ulikuwa
upya wa kweli katika sheria, kwa ajili ya kuiimarisha zaidi sheria iliyokuwepo. Na
kwamba, hoja za Yesu kufanya mabadiliko mapya katika sheria, zilikuwa na nguvu
zaidi kuliko sheria yenyewe ilivyokuwa. Papa alieleza na kutoa mfano wa sheria inahusu
kumchukia adui, badala yake Yesu anasema mwombee mema adui yako. Kumbe basi, hii
inamaanisha Yesu alikuwa akihubiri sheria za kuufikia Ufalme wa Mungu,kwa kufanya
mabadiliko katika maisha kwa kuanzia ndani ya mioyo yetu. Papa alieleza na kuonya
dhidi ya kufikiri kwamba, njia ya Kikristo ni kufanya hiki na kile. . La sivyo. Kuwa
Mkristo ina maanisha kuruhusu kufanywa wapya na Yesu katika njia yake mpya ya maisha.
Na haitoshi kusema , Mimi ni Mkristo mzuri, kila Jumapili, na nashiriki Ibada ya
Misa. Pengine tunafanya hivyo kama mazoea tu ya kila Jumapili, kumbe ndani mwetu mna
imani haba na matendo yetu hayazingatii mafundisho ya Yesu. Papa ameasa maisha ya
Kikristu hayafungamanishwi na mambo ya kidunia lakini ni maisha yanayoongozwa na Roho
Mtakatifu kila wakati , akitufanya wapya katika kuishi na wenzetu . Na haiwezekani
kuyachukua maisha hayo katika mfumo wa vipande vipande na kuacha menginena Ukristu
hauna muda. Wakati wote ni sawa katika mwenendo wake.. na kuwa Mkristo haina maana
mwisho wa maisha ya furaha lakini ni daima ni kama mwanzo wa furaha ya kufanywa upya
na Roho Mtakatifu, au kwa kutumia maneno ya Yesu, kuwa divai mpya."