2013-07-06 15:23:08

Papa aweka tick azimio la kutajwa Watakatifu Yohane XXIII na Yohane Paulo II


Papa Fransisko ameweka sahihi hati yenye azimio la kutaka kuwatangaza kuwa Watakatifu, MwenyeHeri Yohane XXIII na Mwenye Heri Yohane Paulo II.
Padre Federico Lombardi, Msemaji wa Vatican, ijumaa, alitangaza hilo kwa wanahabari mjini , baada ya kutolewa kwa Waraka wa kwanza wa Papa Francisko, juu ya Mwanga wa Imani.
Padre Federico Lombardi alitangaza baada ya Papa Francisko , kukutana na Kardinali Angelo Amato, Mkuu wa Shirika kwa ajili ya Utajaji Wenye Heri na Watakatifu, ambamo Papa alipitisha azimio hilona kuitisha kikao maalum cha Baraza la Makadinali( Consistory) kujadili kwa kina hoja ya kumtangaza kuwa Mtakatifu , Papa Yohane Paulo 11. Na pia alipitisha pendekezo la kuwa na kikao cha kawaida cha Decania ya Makardinali na Maaskofu juu ya kumpandisha katika ngazi ya Utakatifu , Mwenye Heri Yohane XX111.
Akieleza tukio hilo linalo onekana kidogo kama si la kawaida, Padre Lombardi aliwaambia wanahabari kwamba, licha ya kukosekana kwa muuzija wa pili, ni mapenzi ya Papa Francisko kwamba, Utakatifu wa Papa Mkuu wa wakati wa Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican, Yohane XXIII, unatambuliwa rasmi wakati huu maadhiinisho ya miaka 50 ya Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican.
Padre Lombadi pia alieleza kwamba, bado utajaji Utakatifu , unathaminiwa hata bila ya muujiza wa pili kutokea , katika maana kwamba, tayari kuna muujiza wa kwanza ulioongoza Yohane XX111, kutajwa Mwenye Heri. Na pia alitaja uwepo wa majadiliano ya wanateolojia na watalaam,yanayotazama ulazima wa kuwa na miujiza miwili kwa ajili ya mtumishi wa Mungu kutajwa Mwenye Heri au Mtakatifu. Ni wazi, Padre Lombardi aliongeza, Papa anayo mamlaka yote juu ya muujiza wa pili.
Pamoja na hayo, mpaka sasa hakuna tarehe iliyotajwa kwa ajili ya matukio hayo, iwe kikao cha Cosistory au lini watatangazwa kuwa Watakatifu. Padre Lombardi ameonyesha tumaini lake kwamba bila shaka itakuwa kabla ya mwisho wa mwaka.








All the contents on this site are copyrighted ©.