2013-07-04 14:50:47

Papa katika Misa asema, : kukutana na Mungu Hai ni kupitia madonda yake- Vatican


Ili kukutana na Mungu aliye hai ni lazima kwa upole na huruma kubusu madonda ya Yesu , yanayo onekana kupitia ndugu zetu wenye njaa, maskini, wagonjwa , na wafungwa, waume kwa wake. Kusoma, kutafakari na mafungo peke yake havitoshi kutukutanisha na Yesu Kristo aliye hai. Kama ilivyo kwa Mtume Thomas, maisha yetu, yatabadilika tu kwa kugusa madonda ya Kristo, ambayo yanaonekana kwa watu maskini, wagonjwa na wahitaji.
Hili lilikuwa ni fundisho la Papa Fransisko wakati wa Ibada ya Misa mapema asubuhi Jumatano,ibada aliyoigoza katika Kanisa dogo la Mtaktifu Marta, ambayo pia ilikuwa ni Sikukuu ya Mtakatifu Thomas Mtume. Iada hyo ilihudhuriwa na Mapadre kadhaa na wafanyakazi katika Baraza la Kipapa kwa ajili ya Mazungumzo na dini zingine, wakiongozwa na Kardinali Jean-Louis Tauran, Rais wa Baraza.

Homilia ya Papa alirejea somo la Injili , ambamo Yesu anawatokea Mitume wake , lakini Thomas hakuwepo . Papa alisema yalikuwa ni mapenzi ya Yesu kumsubirisha Tomas kwa muda wa wiki moja ili akutane na Yesu. Na baada ya wiki moja Yesu anajitokeza kwa Thomas aliyesema hawezi kuamini hadi yeye Mwenyewe amwone Yesu na ashike madonda yake. Yesu alijitokeza na kumwonyesha madonda yake, mwili wake wote ulikuwa safi, mzuri na wa kuangaza, na madonda yalikuwepo na bado yapo. Tutayaona wakati Bwana atakapokuja mwishoni mwa dunia, ili kwa wale wanao sita kusadiki, basi kama ilivyokuwa kwa Thomas, waweze kuyashuhudia madonda ya Yesu.

Papa alieleza na kusema, kutokuamini kwa Thomas, hadi Bwana kumtaka atie vidole vyake katika madonda kuna tuhakikishia sisi sote kwamba kweli Bwana amefufuka yu hai. Thomas anakuwa mtume wa kwanza kuungamia Umungu wa Kristu baada ya ufufuo, na kumsujudia. ". .

Papa aliendelea kutaja baadhi ya makosa , katika historia ya Kanisa na hasa katika mwendo wa kuelekea kwa Mungu, baadhi waliamini kwamba Mungu Hai, Mungu wa Wakristo hupatikana katika njia ya tafakari. Ni kweli katika tafakari tunapata ufahamu zaidi juu ya maisha ya kiroho. Lakini hili linaweza kuwa jambo la hatari, kama inavyojionyesha historia kwamba wengi waliofuata njia hiyo walipotelea mbali na hawakurudi tena. Kweli ni vyema kufanya tafakari, lakini tafakari peke yake haitoshi kuyaishi maisha yaliyofundishwa na Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, Mtu wa pili katika nafsi Utatu Mtakatifu.Hivyo maisha ya tafakari peke yake ni vizuri na vyema lakini si njia sahihi, ni njia ngumu na haiongozi mahali pa usalamaā€¯.

Papa pia aliangalisha kwa wale wanaodhani kumfikia Mungu ni kupitia njia ya mafugo binafisi, kujinyima na toba. Lakini hata njia hii peke yake haitoshi kukutana na kuishi na Kristu aliye Hai. . Ni sawa na Wapelagians, ambao huamini wanaweza kufika mbinguni kwa juhudi zao wenyewe . Lakini Yesu anatuambia kwamba, njia ya kukutana naye ni katika kuyaona na kuyashika madonda yake.

Kwa namna gani ni kupitia kazi za matendo ya huruma, katika majitolea ya mwili wetu na nafsi pia, kwa ajili ya mshikamano na huduma kwa wahitaji , wenye njaa na kiu, wagonjwa, wanyonge na dhaifu katika jamii, wale walio mahospitalini na majumbani pia ambao wamebeba uchungu wa maisha, wote hao wana alama za madonda ya Yesu Hai Mfufuka.
Leo hii, Yesu anatutaka kupiga hatua mbele katika kumwelekea lakini ni kupitia njia hii ya kuyaona mateso ya watu kama madonda ya Yesu. Tunatakiwa kuyagusa madonda ya Yesu , na kumfariji , kuyafunga madonda yake kwa kitambaa, kwa huruma nyingi na unyenyekevu , tunapaswa kuyabusu madonda ya Yesu. Na hii ni Ishara ya upendo wa Yesu, kama Mtakatifu Frasisko , alivutiwa na mkoma na kubusu miguu yake kwa huruma. . Na ndivyo ilivyotokea kwa Mtume Thomas aligusa madonda ya Yesu na maisha yake kubadilika.

Papa Francis alihitimisha kwa kutoa wito wa kila mmoja , kwamba hakuna haja ya kwenda kusoma tena mafundisho maalum kwa ajili ya kumgusa Mungu aliye hai, lakini ni kuingia mitaani na kuhudumia wenye kubeba madonda ya Yesu kwa upole na ukarimu . Ni wote kutoka nje mitaani na kumgusa Yesu aliyefichana katika mahangaiko ya watu wahitaji. Papa aliomba Neema ya Mtume Thomas, ambaye kwa ujasiri aliyagusa madonda ya Yesu na kusadiki na kumwabudu Mungu aliye Hai.








All the contents on this site are copyrighted ©.