2013-07-04 12:20:52

Jaji mkuu wa Mahakama kuu aapishwa kuwa Rais wa kipindi cha mpito Misri!


Bwana Adly Monsour, aliyekuwa Jaji mkuu wa Mahakama kuu ya Misri ameapishwa rasmi siku ya Alhamisi kuwa Rais wa Misri katika kipindi cha mpito, hadi hapo uchaguzi mkuu utakapofanyika tena, baada ya Jeshi kumwondoa kutoka madarakani Rais Mohammed Morsi. Hadi sasa tarehe rasmi kwa ajili ya uchaguzi mkuu bado haijapangwa.

Jeshi limeamua kujitwalia madaraka baada ya mamillioni ya wananchi wa Misri kuandamana kutaka Rais Morsi kujiuzuru kutoka madarakani, lakini akagoma kutekeleza sauti ya umma!







All the contents on this site are copyrighted ©.