2013-07-04 08:32:12

Historia fupi ya wito wa Shemasi Delphinus Felician S. Mwemezi, SDB


Askofu msaidizi Titus Joseph Mdoe wa Jimbo kuu la Dar es Salaam hapo tarehe 5 Julai 2013 anatarajiwa kutoa Daraja Takatifu la Upadre kwa Mashemasi wa Jimbo kuu la Dar es Salaam: Shemasi Cletus Mzeru, Shemasi Henry Marine Kachelewa na Shemasi Justus Rugaimukamu. Kutoka Shirika la Wakarmeli ni: Shemasi Paul Domician Malewa, Shemasi Victor Alphonce Biramata pamoja na Shemasi Paschal James Shirima. RealAudioMP3
Shemasi Delphinus Mwemezi wa Shirika la Wasalesiani wa Don Bosco ni kati ya Mashemasi watakapewa Daraja Takatifu la Upadre, wakati huu Mama Kanisa anapoadhimisha Mwaka wa Imani kwa Majandokasisi na Wanavosi, jeuri na matumaini ya Kanisa. Shemasi Delphinus Mwemezi anatushirikisha sehemu ya historia ya maisha na wito wake
Mimi ni shemasi Delphinus Felician Stanslaus – Mwemezi (mwana shirika la Wasalesiani wa Don Bosco), nimezaliwa katika familia ya watoto nane, tukiwa watoto wa kiume wanne na watoto wa kike wanne. Wazazi wangu kwa majina ni: Baba Felician Mwemezi Stanslaus na Mama Genoveva Yoakim Rwechungura, wote ni wazaliwa wa Bukoba – Kagera, Mama ni Mzaliwa wa kijiji cha Muutwe na Baba ni Mzaliwa wa kijiji cha Katoma- Kamachumu.
Baba na Mama walifunga pingu za maisha kama mke na mume tarehe 22.10.1974, katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Magomeni, Jimbo kuu la Dar-es-salaam. Ili tokea hivyo kwa sababu kwa miaka mingi waliishi Dar-es-salaam, huko Ubungo, Baba akiwa mtumishi wa serikali, kisha akawa kama mfanyabihashara binafsi. Wote Baba na Mama kama wazazi wetu wamekuwa mfano bora wamaisha ya kikristo na maisha ya familia. Kweli ilitokea kuwa tangu utotoni familiya ya Baba yangu mzazi na Mama yangu mzazi zimekuwa na misingi mizuri ya maisha ya kikristo, tokea kwa mababu zetu. Kwanza, Babu yangu kwa upande wa Mama alikuwa Kateskista mzuri katika Parokia ya Kagondo Jimbo Katoliki Bukoba.
Leo ninapo simama kama Mkristo na Shemasi naona kuwa misingi bora ya maisha yangu ya Kikristo imeanzia mbali, kuanzia kwa familia yangu. Wazazi wangu ni watu wa imani, kila jumapili walihakikisha sisi kama watoto wao, tunashiriki Ibada ya Misa Takatifu, pia nikiangali jinsi walivyo simamia maisha yetu ya Kisakramenti, kuanzia sakramenti za mwanzo, ubatizo, ambamo sisi wote kama watoto wa familia ya Mzee Felician Mwemezi tulibatizwa tukiwa wachanga, wazazi walijua kuwa Sakramenti hii ni muhimu pamoja na sakramenti zingine, hivyo leo najivunia sana wazazi wangu, waliotusindikiza katika maisha yetu ya imani, mpaka tulipokuwa watu wazima, mpaka leo hii. Mimi kama mtoto wao watatu, nina dada na kaka zangu ambao wanaishi maisha yao ya Kikristo vyema katika wito wao wa maisha ya ndoa. Kweli ni jambo la kujivunia sana.
Ninapo simama hapa kama shemasi kweli, jambo hili linanipeleka mbali sana, katika fikra, na tafakari juu ya zawaidi hii ya wito wa kitawa na kipadre, kweli ni safari ndefu na watu wengi wamenilea na kunishika mikono na baadhi yao wameacha alama katika maisha yangu, kama nilivyoanza kwa kuongelea kuhusu wazazi wangu na familia yangu kwa ujumla, Leo natambua zaidi kuwa wito wowote uanzia katika familia, familia zinazotoa mifano kwa watoto zao wake kwa waume. Hivyo miito mitakatifu inapata chimbuko lake katika familia.
Kweli katika UTOTO WANGU, sikujua nini Mungu alitaka toka kwangu katika maisha yangu ya ukubwani, ninachojua utotoni, nilipenda sana kuiigiza mapadri, nikijufunga mashuka kama chasuble, lakini ilikuwa ni tutoto, mpaka siku moja dada yangu na kaka yangu waliniambia, mimi natakakuwa Padre, lakini ilikuwa ni utoto.. Nakumbuka mwaka jana nilipopata ushemasi na kwenda nyumbani kwa likizo, dada yangu alinikumbusha ili jambo.
Sasa mimi nilikua tu kama watoto wengine ndani ya familia, nikasoma Dar-es-Salaam katika shule ya “Ubungo National Housing”, kweli nilipenda kuhudhuria vipindi vya dini sana, kila tulipokuwa tunapata nafasi. Basi kulikuwa na PADRE Joseph kutoka Parokia ya Manzese, alikuwa karibu sana nami pamoja na familia yangu, akanihamasisha kuwa mtumishi wa Altare. Siku moja nilipo kuwa darasa la sita, aliamua kuniuliza kama nigependa kwenda kusoma katika Seminari ndogo baada ya masomo yangu ya shule ya msingi, basi bila kusita nilimwambia sawa, lakini lazima tuongee na wazazi wangu.
Baada ya siku chache, MWAKA 1992, nilipokuwa darasa la saba, akaniambia nichague seminari nayotaka kwenda, alionyeshaorodha ndefu ya seminari ndogo za Tanzania, lakini mimi bila kufahamu mpango wa Mungu, nikajikuta nachagua, DON BOSCO SEMINARY MAFINGA, Iringa, akaniambia sawa, nikarudi nyumbani, nikawaeleza wazazi, wakasema sawa naweza kuandika barua ya maombi, nikafanya hivyo, nikapeleka kwa Padre Joseph, kisha akazituma kwa njia ya Posta. Basi tutakaa baada ya miezi michache, nikapata mwaaliko wa kwenda kwa mtihani pamoja na kufanya mahojiano huko Don Bosco Seminary Mafinga kwa wiki moja. Nilifurahi sana, kwa sababu mimi hupenda sana kusafiri.
Basi wazazi wangu wakaniandalia vifaa vilivyohitajika, kwa sababu kilikuwa kipindi cha baridi huko Mafinga, kwa mara ya kwanza nikasafiri pekee yangu, kwenda Mafinga, lakini kwenye hiyo Bus ya Lupelo nilimkuta rafiki yangu Bonventura Mathias, ambaye tulikuwa tunakutana Parokiani, basi tukasafiri wote mpaka Mafinga, tukafika huko na tukakuta Mapadri wa Shirika la Mtakatifu Don Bosco wanatusubiri, kweli tuka kaa huko wiki moja, kwa masomo na mtihani na michezo mbali mbali.

Maana mimi utotoni mwangu nilipenda sana muziki, basi baada ya wiki moja tukarudi nyumbani, lakini hile experience, ilibaki sana ndani ya roho yangu, nikawa nasubiri kujua kama nimeshinda, mpaka siku moja nikaota nimeitwa huko kwa kuendelea na masomo Don Bosco Seminari, kweli baada ya siku chache nilipokea barua ya kuitwa kwenda kujiunga na seminary hiyo, Nilifurahi sana, nikawaeleza wazazi nao wakafurahi na wakakubali lipa ada zote, maana seminarini ada ilikuwa juu kuliko shule za serikali, kweli nikaenda kuaanza maisha ndani ya Don Bosco Seminari Mafinga.
Kweli nilipenda sana maisha ya seminari, niliona mkono wa Mungu, katika masomo na kazi nyingine hasa katika malezi ya kiroho. Mapadri walikuwa sana karibu nasi, kitu ambacho kilikuwa si cha kawaida, lakini kwa sisi Wasalesiani wa don Bosco ni muhimu na ni kawaida, basi kuanzia MWAKA 1993-1997, Nilisoma huko Pre-form one mpaka form IV. Kweli Mungu aliniangazia sana, na kunipa nguvu za kushida yote mepesi na magumu, nilivyomaliza form IV, nikajadiliana na familia yangu, nikawaambia nigependa endelea na seminari, kwa masomo ya form V ana Form VI, huko Salesian Seminari Dodoma, bila kusita wazazi walikubali kugharamia ada zote, hivyo tena nikaacha nafasi yangu ya shule ya serikali na kuingia Salesian Seminari Dodoma.
Mwaka 1998 -2000, kweli kilikuwa kipindi kizuri cha kuendelea kutafakari zaidi kwa maana sasa nilikuwa mtu mzima zaidi, pia nilikuta walezi wazuri pia, nakumbuka Gombera wangu alikuwa Padri Dominic PD . Kweli alinilea vizuri kama Baba wa kiroho, pamoja na mapadri wengine. Maisha yaliendelea vizuri kadri Mungu alivyotaka.
Mwaka 2000 nikamaliza Kidato cha VI na kufahuru vizuri, kweli kwa msaada wa Mungu na tafakari na kushirikiana na walezi pamoja na familia yangu, niliamua kungia kwa Pre-Novitiate – Bosco Boys Nairobi Kenya, kweli maisha yaliendelea, sasa nilikuwa napata picha kamili kuhusu njia mbayo nilikuwa ninafuata kadri ya mapenzi ya Mungu, basi kwa msaada wa Mungu na walezi, niliweza kueendelea vizuri, na mwaka 2001 Agosto nikaingia hatua ya Unovisi HUKO DEBREZEIT –ETHIOPIA baada ya tafakari, kisha 15Agosto niliweka nadhiri zangu za kwanza kama mwanashirika wa Shirika la Wasalesian wa Don Bosco, huko Debrezeit Ethiopia. Hapa tulisaidiwa kukua na kukomaa katika maisha na wito wetu kama Wanashirika wa Don Bosco.
Mwaka 2002 – 2005 nilingia katika masomo ya FALSAFA, kweli huu ni uwanja mwingine wa malezi, Basi nilijiunga na chuo chetu cha Falsafa na Elimu huko Moshi ( Don Bosco College of Filosophy and Education affiliation of the Catholic University of Eastern Africa - CUEA). Kweli nilipenda sana miaka hiyo niliyo ishi hapo chuoni, pamoja na walimu wazuri wa falsafa, Gombera wangu alikuwa ni mtu mwema sana na mlezi bora, Fr. Joseph Pulickkal, SDB, na wengine walio kuja baada yake, kweli miaka hii ilikuwa ni miaka ya kukomaa KIROHO NA KIFIKRA, KWELI NILIPENDA SANA FALSAFA MPAKA LEO HII.
Nilijaribu kuingia kiundani na kujua mawazo tofauti tofauti ya wanafalsafa mbali mbali, na kumbuka Prof. wangu Padre Selvam, alikuwa ni changamoto sana kwangu, na alinifanya nisome sana, na kuamsha akili yangu zaidi, siyo tu kwa mawazo ya kifalsafa bali akili yangu kumwelekea Mungu ambaye ananishirikisha utashi wake, kisha nilikutana na Prof. Eustace Siame SDB, toka Zambia na yeye alikuwa changamoto kwangu, kweli walinisaidia kukomaa kimawazo na kujua kuwa Mungu ni Mungu, na abaki kuwa Mungu, ata katika falsafa, God is beyond all these, He is our true knowledge.
Basi MWAKA 2005 nikahitimu, masomo yangu ya falsafa vizuri na wakuu wa Shirika letu kufuatana na mahitaji ya Shirika letu kwa upande wa Afrika Mashariki, waliamua kunituma kusoma tena Falsafa katika Chuo kikuu cha Kikatoliki Afrika Mashariki – (The Catholic university of Eastern Africa – CUEA), basi nikaenda huko toka mwaka 2005-2007, kweli Chuo ni kizuri na kinamambo mengi, lakini Mungu alikuwa nami, pia sasa ilikuwa ni ngazi ya juu, kwa maana nilikuwa nachukua shahada ya pili ya Falsafa, kweli nilimtegemea Mungu katika yote, naniliona mkono wake katika kazi zangu zote na maisha yangu.

Mwaka 2007, nilimaliza kisha wakubwa zangu na walezi wangu wakanituma nirudi Moshi,Tanzania katika chuo chetu cha Falsafa na Elimu,nilirudi huko na kuaanza kufundisha falsafa toka MWAKA 2007-2009. Kweli ilikuwa ni miaka mizuri sana kwangu, kuishi pamoja na Waselesian wengi, Wakufunzi na Wanafunzi, kweli nakumbuka miaka hiyo miwili kwa furaha sana.
SASA MWAKA 2009, ulikuwa ni mwaka muhimu sana, kwa sababu niliweka nadhiri zangu za daima kama msalesiani wa don Bosco., kweli ulikuwa ni wakati mzuri wa neema, na kutafakari yote Mungu aliyo nitendea, nakumbuka ujumbe katika card ya mwaliko,“Lord to who shall we go, you alone have the words of eternal life (Jn 6, 68) . Nilikuwa mimi na wenzangu wengine watatu tulio soma wote ( Fr. Richard Mtui na Fr. Mathias Isaka hawa tulisoma wote toka tukiwa seminari ndogo), Kisha mwingine alitukuta salesian Seminari Dodoma Fr.Oswin Ndowa, Nawashukuru sana hawa Waselesiani wenzangu wamekua sana karibu nami.
MWAKA 2009, Mkubwa wangu wa Kanda ya Afrika Mashariki, alinituma nijekufanya malezi yangu ya taalimungu hapa Roma kwenye Chuo Kikuu cha Kipapa cha Wasalesiani wa Don Bosco. Nimekuwa hapa kwa miaka minne sasa, lakini namshukuru Mungu kwa yote.
KISHA MWAKA 2012 ulikuwa mwaka wa pekee kwa maana kwa neema za Mungu nilipata ushemasi, hapa Roma katika Kanisa letu la Moyo Mtakatifu wa Yesu ( Basilica del Sacro Cuore di Gesu’), hiyo tarehe 23Juni2012, ilikuwa siku ya pekee sana katika maisha yangu, na ninazidi ona matendo makuu ya Mungu.
Na sasa tarehe 05 Julai 2013, itakuwa siku nyingine ya pekee katika maisha yangu, kweli, ni siku ya furaha na ni siku ya kuona maisha yangu, na kumshukuru Mungu kwa yote, kweli Mungu, amenitoa mbali, na hii inanifanya kufikiria baadhi ya maandiko matakatifu: “Nifanye Mapenzi yako ee Mungu: ndiyo furaha yangu” ( Zab 40:8); “Mimi ni nani ee Bwana Mungu hata umenifikisha hapa” (2Sam 7:18); “na Basi, sasa na idumu imani, tumaini na upendo...” (1Cor 13:13).
Sasa kwa kumaliza tafakari yangu, napenda sema kuwa Mungu ni mwema kila wakati, na Mungu anapenda kanisa lake siku zote. Nimejaribu toa kiufupi huu ujumbe juu ya wito wangu, Naamini kuwa nilipofikia siyo kwa nguvu zangu za kibinadamu, bali ni mkono wa Bwana aliye niongoza na anayeniongoza mpaka sasa, yeye ni Mchungaji Mwema. Nakupitia watu, kama vyombo vyake, ameweza nishika mkono na kuniongoza.
Kweli itakuwa ni furaha kubwa siku hiyo ya tarehe 05JULAI 2013, nitakapopewa daraja hili takatifu la upadrisho na Baba Askofu Titus Joseph Mdoe, Askofu Msaidizi wa Jimbo kuu la Dar-es-salaam, huko katika Parokia ya Mbezi Luis.
Ujumbe wangu Mkuu katika upadrisho wangu, katika card za mwaliko na souvenir in: “ MCHUNGAJI MWEMA HUUTOA UHAI WAKE KWA AJILI YA KONDOO WAKE (YON: 10,11).
Kweli ni ujumbe utakao niongoza katika maisha yangu ya kumtumikia Mungu na watu wake
Naomba Mungu anijalie hii neema ya kuweza kutoa nguvu zangu zote, na maisha yangu yote na uhai wangu wote kwa ajili ya kumtumikia yeye na watu wake.
NAPENDA KUSEMA KUWA KATIKA SAFARI YANGU YA WITO HUU, KUMEKUWA NA VITU NA MAMBO MENGI MAZURI, LAKINI PIA KUMEKUWA NA CHANGAMOTO, NYINGI ILA MUNGU AMEKUWA UPANDE WANGU NA MIMI NAMTEGEMEA YEYE DAIMA, HAKUNA MAISHA AU WITO SIYO KUWA NA CHANGAMOTO, CHANGAMOTO NI SEHEMU YA MSALABA, HAKUNA KUJITOLE BILA MSALABA, NA HAKUNA UFUFUKO BILA IJUMAA KUU.
Naomba sana sala zenu mnisindikize katka kuijongea Altare ya Bwana.









All the contents on this site are copyrighted ©.