2013-07-03 11:20:45

Padre Appolinaire Mwenyekiti wa Tume huru ya uchaguzi DRC asimaamishwa uongozi


Baraza la Maaskofu Katoliki Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Congo, katika taarifa yake mara baada ya kumaliza mkutano wake mkuu, linasema kwamba, Padre Apollinaire Malumalu ameondolewa kutoka kwenye madaraka ya mkurugenzi mkuu wa Jukwaa la Kardinali Martino Barani Afrika kwa kujihusisha na masuala ya kisiasa na hatimaye, kuchaguliwa kuwa ni Mwenyekiti wa Tume huru ya uchaguzi nchini DRC kinyume cha sheria za Kanisa.

Padre Malumalu alichaguwa katika wadhifa na Bunge la DRC hapo tarehe 7 Juni 2013. Mapema Baraza la Maaskofu Katoliki DRC lilipiga marufuku Mapadre na watawa kujiingiza katika masuala ya kisiasa au kukubali kushika nyadhifa za uongozi serikalini.







All the contents on this site are copyrighted ©.