Mshikamano wa Vatican na wananchi wa Afrika ya Kati
Kardinali Fernando Filoni, Msimamizi wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Uinjilishaji
wa Watu, mapema Jumatatu alimpokea , Askofu Mkuu Dieudonné Nzapalainga wa Jimbo Kuu
la Bangui, akiwa amefuatana na kundi la la waamini ishirini, waliomsindikiza katika
Ibada ya kuvalishwa Palium na Papa Fransisko. Ibada iliyofanyika Jumamosi Juni
29 katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, ikienda sambamba na Siku Kuu ya Kiliturujia
ya Watakatifu Petro na Paulo . Kwa mujibu wa taarifa ya fides, baada ya mkutano
wa faragha na Askofu Mkuu Nzapalainga, Kardinali Filoni alikutana pia wa kundi la
waamini. Katika hotuba yake aliwatia moyo dhidi ya hali ngumu ya maisha kama kanisa,
yanayopita katika kipindi hiki hasa baada ya kuangushwa kwa utawala wa Rais Bozize.
Alitaja ukaribu kiroho na mshikamano unaoonyeshwa na Shirika la Kipapa kwa ajili
ya Uenezaji imani, kwa watu nzima katika Afrika ya kati, na matumaini ya baadaye
yake katika upatikanaji wa amani ya kudumu. Kardinali alikumbuka pia ziara yake
ya kichungaji aliyoifanya mwaka jana Julai Afrika ya Kati, ambako aliwaweka Wakfu
Maaskofu wapya wanne, ikiwa ni pamoja na Askofu Mkuu wa Bangui. Kardinali alisisitiza
kwamba Kanisa katika Jamhuri ya Afrika ni kati ya maeneo yanayotazamwa kwa makini
na Shirika kwa ajili ya Uinjilishaji wa watu, na linakusudia kuendelea kusaidia ukuaji
wa kanisa na kukufanya upya kwa ajili ya kufanikisha ukomavu zaidi. Na kwa niaba
ya waamini, Godefroy Mokamanede Francis alimshukuru Papa kwa maombi na baraka zake
kwa ajili ya neema ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, aliyoyatoa wakati wa sala ya Malaika
wa Mbingu , Jumamosi Juni 29. Na pia alitoa shukurani kwa Kardinali Filoni , kwa
kuwa na nafasi ya kukutana nao. Katika hotuba yake, hakusahau kutoa sauti ya kilio
cha watu wa CAR, ambao kwa wakati huu wanapambana na hali ngumu halisi za jamii
kutojali maadili ya maisha iwe kijamii, kisiasa na kidini pia , hali inayowatia watu
wenye mapenzi hofu na wasiwasi juuya mustakabhali wa jamii na maslahi mengine
katika taifa hilo. Kardinali akiagana na ugeni huo, aliwahakikishia wao si peke
yao. Kanisa lote ni pamoja nao. Kisha aliwahimiza daima kuwa wajenzi wa amani na
haki. Na aliwazawadia wote, Rosari iliyobarikiwa na Baba Mtakatifu akiwaomba watoleee
maombi yao kwa Mama Yetu wa Afrika, na wafikishe baraka la Papa walizopokea kwa waaamini
wote , huku akionyesha tumaini kwamba watakutana tena siku zijazo.