Wake wa Marais wa Marekani wapania kuwajengea uwezo wanawake wa Afrika!
Mama Michelle Obama na Mama Laura George Bush wa Marekani, wameamua kuunganisha nguvu
zao ili kuwekeza kwa wanawake Barani Afrika, ili kuwajengea uwezo wa kiuchumi pamoja
na kupambana fika na changamoto za maisha.
Hizi ni juhudi ambazo zinafanywa
kwa mara ya kwanza na wanawake wa Marais hawa wawili wa Marekani, kama sehemu ya mchakato
wa kuendeleza mafanikio yaliyopatikana chini ya uongozi wa Rais George W. Bush wa
Marekani hasa kampeni dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi Barani Afrika. Uamuzi huo umefikiwa
na wanawake wa Marais wa Marekani muda mfupi tu kabla ya kufanya kumbu kumbu kwa watu
walioathirika kutokana na vitendo vya kigaidi kwenye Ubalozi wa Marekani, Jijini Dar
es Salaam kunako mwaka 1998.
Mfuko wa Bush unasaidia sana katika mchakato
wa maboresho ya afya ya wanawake Kusini mwa Jangwa na Sahara na katika Nchi za Amerika
ya Kusini.