2013-07-02 11:14:51

Ratiba elekezi kwa Mwezi Agosti 2013


Baba Mtakatifu Francisko kwa Mwezi wote wa Agosti, hataweza kutoa Katekesi zake kwa Siku ya Jumatano hadi tarehe 4 Septemba 2013. Katika mwezi Agosti, Baba Mtakatifu ataendelea kusali na waamini pamoja na mahujaji watakaofika kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro, mjini Vatican.

Taarifa inaonesha kwamba, Baba Mtakatifu tarehe 15 Agosti 2013, katika Maadhimisho ya Siku kuu ya Bikira Maria Kupalizwa Mbinguni, ataadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwenye Ikulu Ndogo ya Castel Gandolfo, nje kidogo ya mji wa Roma, baadaye, atasali pamoja na waamini Sala ya Malaika wa Bwana. Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican itaendelea kukujuza yale yatakayokuwa yanajiri mjini Vatican na sehemu mbali mbali za dunia! Waswahili wanasema, "Stay Tuned".







All the contents on this site are copyrighted ©.