Tamko kutoka Ofisi ya Habari ya Vatican juu ya yanayoendelea katika Idara ya Fedha
ya Vatican (IOR), linaeleza kwamba, aliyekuwa Mkurugenzi wa IOR, Paolo Cipriani
na Naibu Mkurugenzi Massimo Tulli wametoa hati za kujiuzuru kutoka nafasi zao, baada
ya utumishi wa muda mrefu. Wametaja sababu za kujiuzuru kwao kwamba, ni kwa manufaa
ya Taasisi hiyo na Jimbo Takatifu.
Baraza la Usimamizi la tume hiyo na Tume
ya Makardinali inayohusika na masula ya fedha na uchumi wa Vatican, wamekubali kujiuzulu
kwao. Vivyo hivyo tume iliyoteuliwa hivi karibuni na Papa , imekubali uamuzi huo.
Katika nafasi zao wameteuliwa Rais waTume Ernst von Freyberg, kuwa pia Mkurugenzi
Mkuu wa Muda, kazi anayoianza mara moja, na jopo la udhibiti la AIF Vatican, limekubali
taarifa hiyo.
Ernst Freyberg von atatenda kwa kusaidiana na Rolando Marranci
kama kaimu Naibu Mkurugenzi na Antonio Montaresi anachukua nafasi ya Afisa Mkuu
wa Tahadhari, na msimamizi wa miradi maalum. Hapo awali Rolando Marranci aliwahi
kuwa Afisa Uendeshaji Mkuu katika benki moja ya Italy iliyoko London. Na Antonio
Montaresi aliwahi kuwa msimamizi na Afisa Mkuu wa Mwafaka na benki mbalimbali nchini
Marekani. Taasisi ya Fedha ya Vatican , IOR, ilianzishwa mwaka 1942 kwa maamuzi
ya Papa . Madhumuni ya IOR ni kuhudumia Jimbo Takatifu na Kanisa Katoliki duniani
kote, kama inavyoelezwa katika Katiba yake. IOR hutunza mali za vikundi , taasisi
na mashirika yenye kutambulika kisheria na yenye kuhusiana na Kanisa la Katoliki
kama inavyoelezwa kisheria na Vatican. IOR, ina wafanyakazi 114, na ni peke ambayo
ofisi zake zilijengwa ndani ya nchi ya Vatican.