Mkristu anatakiwa kubaki shujaa licha ya udhaifu wake
Wakristu wametakiwa kubaki imara katika imani na kuachana na hofu na woga wa kuachana
na dhambi. Wanatakiwa kuwa jasiri katika kupambana na mawimbi ya majaribu ya dhambi
yanayo taka kuudhoofisha moyo.Ni wito wa Papa Fransisko, wakati akiongoza Ibada
ya Misa, mapema Jumanne katika kanisa dogo la Mtakatifu Marta ndani ya Vatican.
Papa
amesema kwamba, tunapaswa kutambua kwamba, sisi ni dhaifu na hivyo ni lazima kuikimbia
dhambi bila kutazama mazoea mabaya ya nyuma. Katika Ibada hiyo , Papa aliiongoza
akisadiana na Kardinali Manuel Monteiro de Castro, na Mapadre Kadhaa. Pia ilihudhuriwa
na Walei wafanyakazi wa Mahakama ya Kitume ya Kitubio na kundi jingine kutoka la
Chuo cha Kipapa cha Kikanisa.
Katika homilia yake Papa alitafakari juu
ya masomo ya siku , akiangalisha katika mapambano ya kiroho dhidi ya dhambi , na
kuainisha mambo manne katika masomo hayo kwamba , kuna utendaji wa kutenda polepole,
kuna kuyaangalia ya nyuma, kuwa na hofu na kurejea kwa Bwana kwa neema ya Roho Mtakatifu.
Papa Fransis, ameyaangalia hao katika mtazamo wa uwezekanavyo wa kujikwamua
na mapambano ya kiroho na matatizo mengine. Papa alianza kwa kutazama tabia ya
kutenda polepole katika kuyaacha ya nyuma, kama ilivyokuwa kwa Lutu aliyeamuriwa kuondoka
katika mji kabla haujaharibiwa , lakini akafanya hivyo polepole kwa kinyongo. Malaika
anamharakisha kukimbia, lakini yeye ndani yake hana uwezo huo wa kukimbia kutoka
uovu na dhambi, kwa kuwa ana yatamani ya nyuma yanayoangamiza. Na ndivyo ilivyo
hata kwetu leo hii, tunatakiwa kwenda nje ya dhambi , lakini tunapata kigugumizi kuamua
hivyo, kwa kuwa tunayatamani yale yanayoangamiza, tunavutwa nyuma badala ya kwenda
mbele, kama ilivyokuwa katika majadiliano kati ya Malaika na Lutu.
Papa anasema
ni jinsi gani ilivyokuwa vigumu kujitenga na dhambi. Ni vingumu pia kushinda majaribu
, lakini Sauti ya Mungu inatuambia katika neno lake , kimbia, huwezi kupambana na
moto wa dhambi wenye kukuua. Pia Mtakatifu Tereza wa Mtoto Yesu, alifundisha, wakati
mwingine, katika majaribu , suluhu pekee ni kutafuta namna ya kutoroka. Hakuna sababu
za kuonea aibu kutoroka. kutoroka niujasiri, ni kutambua kwamba, sisi ni dhaifu na
hivyo inabidi kutoroka kabla dhambi haijatumaliza. Na mahali pekee pa kutorokea ni
katika njia ya Yesu.
Papa alieleza na kukemea udhaifu wa kuyatazama ya nyuma
kama alivyofanya Lutu. Na ametaja njia inayofaa kumaliza hamu ya kurudia dhambi ,
kukumbuka vinono vya kulaghai vilivyowekwa juu ya meza ya dhambi, na mauti, ni kuukaza
uso kwa Bwana, na kusema, sirudi nyuma. Ni kutazama ya mbele tu na kupiga hatua katika
mwendo huo bila ya kuyafikiri yaliyopita.
Papa amekiri udhaifu wa binadamu
akisema sisi sote ni dhaifu , na hivyo, kwa utambuzi huo, ni lazima kuwa na ujasiri
wa kujilinda dhidi ya udhaifu huo. Kwa namna gani ni kukimbilia msaada wa Bwana na
kumwambia , Bwana nina zama, niokoe, kama ilivyokuwa kwa wanafunzi wa Yesu, walipopigwa
na mawimbi makali baharini , walimwamsha Bwana na kusema Bwana tuokoe tunaangamia.
Walikuwa na hofu. Na hofu hiyo ni majaribu ya shetani, ni kuwa na hofu ya kusonga
mbele katika njia ya Bwana.
Papa anasema, kuna majaribu mengi , kama ilivyokuwa
kwa wana wa Israel wakati wa kukombolewa katika utumwa , walifika mahali wakasema,
heri utumwa wa Misri. Walishikwa na hofu za kusonga mbele. Ni woga na kukata tamaa.
Papa
amewatia shime Wakristu akisema, hakuna sababu ya kuongoza au kukata tamaa. Lete
hofu zako zote kwa Yesu anayewaaambia wafuasi wake , msiogope. Msiogpe hofu haina
msaada kwetu. Msaada wetu, ni neema ya Roho Mtakatifu.
Papa ameonya daima,
kabla ya dhambi kutenda dhambi na mbele ya hamu ya kutenda dhambi, huwa kuna hofu
fulani inayoonya, usipoteze nafasi hiyo, wahi kw akutafuta msaada wa Bwana, mwite
nayemara moja atakujibu. Sema Bwana naangamia, nae atakusadia.
Na kwamba
kweli sisi sote ni dhaifu, lakini ni lazima tuwe jasiri kupambana na udhaifu huo.
Na ujasiri wetu hupata nguvu kwa kukataa kutazama ya nyuma, ni kuyakimbia, na wala
tusikubali kuzama katika hamu za mambo ya nyuma au mazoea mabaya. "Usiogope, daima
kaza uso wako kwa Bwana! "