2013-07-01 16:44:23

Waraka wa kwanza Kitume wa Papa Fransisko kuwasilisha Ijumaa wiki hii


Waraka wa kwanza wa Kitume wa Papa Fransisko ni juu ya Mwanga wa Waamini( Lumen Fidei)
Mkuu wa Dekania ya Maaskofu Kardinali Marc Oullet , Askofu MKuu Gerhard Ludwig Muller, na Mkuu wa Shirika kwa ajili ya Mafundisho Sadikifu na Mkuu wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Ukuzaji wa Uinjlishaji mpya Askofu Mkuu Rono Fischella, Ijumaa ijayo watawasilisha Waraka wa Kwanza wa Kitume, Papa Fransisko, mbele ya Wanahabari. Waraka wenye jina Lumen Fidei. Wanahabri wote wenye dhamana Vatican mnaalikwa kufika katika ukumbi wa Yohane Paulo 11 wa Ofisi ya Habari ya Vatican, majira ya saa sita kamili , Ijumaa tarehe 5 Julai 2013. .
Waraka huo umeandikwa katika lugha ya Kiitaliano, Kiingereza Kifaransa , Kijeruman, Kihispania na kireno pia.










All the contents on this site are copyrighted ©.