2013-07-01 09:54:46

Dar es Salaam hapatoshi: Rais Obama na Bush wametinga timu!


Rais Barack Obama wa Marekani na Rais mstaafu George Bush wa Marekani wako nchini Tanzania kwa shughuli tofauti. Rais mstaafu Bush yuko nchini Tanzania ili kushiriki katika mkutano wa Taasisi yake unaopania kuwajengea uwezo wanawake katika sekta ya elimu, afya na uchumi na maendeleo. Rais mstaafu Bush anatarajiwa kuzungumza na wanawake kutoka Tanzania, Jumanne, baada ya Rais Barack Obama kuhitimisha ziara yake nchini Tanzania.

Wachunguzi wa masuala ya kisiasa wanasema, uwepo wa Rais Obama na Bush kwa pamoja Jijini Dar es Salaam ni kielelezo makini kwamba, Marekani inawajali wananchi wa Afrika na wanataka kusaidia katika mapambano dhidi ya ujinga, maradhi na umaskini. Itakumbukwa kwamba, Rais mstaafu George Bush alisaidia sana katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi Barani Afrika, juhudi zinazoendelezwa na Rais Obama.

Akizungumza na waandishi wa habari, Rais Obama amesikika akisema kwamba, ukata na sera za Marekani zinamnyima uhuru wa kuweza kulisaidia Bara la Afrika, lakini msaada unaotolewa na Marekani kwa sasa unaweza kuleta mabadiliko makubwa kwa wananchi wa Afrika.







All the contents on this site are copyrighted ©.