2013-06-29 13:35:22

Mwaka wa Imani: Utamadunisho katika maisha mchanganyiko na imani zingine


Katika azimio la kazi za misioni za Kanisa lililoandikwa katika Mtaguso Mkuu wa Pili w a Vatican linasema, "Kanisa limetumwa na Mungu kwa mataifa yote, ili liwe sakramenti ya wokovu kwa wote na hivyo hudaiwa uwajibikaji wa ndani kwa ukatoliki wake , na kwa kulitii agizo la mwanzilishi wake, linafanya bidii ya kuitangaza Injili kwa watu wote".

Aidha Mtaguso Mkuu ulizitazama hali za nyakati hizi ambamo mnajionyesha hali mpya za mabadiliko katika maisha ya ubinadamu na kuona haja ya Kanisa kuwa chumvi ya dunia na nuru ya ulimwengu, inakuwa ni hitaji la lazima zaidi, kufanya mabadiliko mapya hasa katika imani , ili binadamu aweze kujumuika pamoja kama familia moja na taifa moja la Mungu. Ni wazi kwamba, Azimio la Mungu kwa ajili ya wokovu wa binadamu wote halitimizwi kisirisiri, kwa juhudi tu za kibinadamu au kwa njia ya juhudi za kidini peke yake, lakini ni katiika uweza na mpango wa Mungu mwenyewe , hasa katika kuwagusa wale wanaomtafuta Mungu wa Kweli , kwa namna nyingi.

Aidha tamko la Kanisa juu ya uhusiano wa Kanisa na dini zisizo za Kikristo linasema, tangu zamani za kale mpaka leo pamekuwepo katika mataifa yote, hisia juu ya uwezo usioonekana ambao upo katika mkondo wa mambo na matukio ya maisha ya kibindamu. Pengine hutambulika kama ni uwezo wa Ukuu wa Mungu, ambaye huadhimishwa na amepewa majina mbalimbali na wengi humwita Baba au Mkuu. Hizi ni hisi za utambuzi zinazo jipenyeza katika maisha ya watu, ambazo ni hisia za kidini.

Mtaguso Mkuu wa Pili Vatican unaendelea kuzitaja hisia hizi za kumtafuta Mungu , ukifanya rejea katika maneno ya Yesu : Tafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na haki yake (Mt 6:33)na kutao tafasiri kwamba, hii inamaanisha mawazo yetu na nguvu zetu zijue zinako elekea, bila kusahau maneno mengine ya Bwana yanayosema, ” mengine yote mtapewa kwa ziada.

Na hivyo Kanisa litambua tangu mwanzo wa binadamu na hata sasa, bado kuna watu wanaoendelea kumtafuta Mungu wa ukweli kwa nguvu zao zote. Na ndivyo ilivyo katika maisha haya mchanganyiko ya kijamii. Kuna watu wenye tabia na miono mbalimbali katika maisha ya kila siku . Hao ndiyo Waamini wa Kristu wanapaswa kukutana nao na kuwafahamisha juu ya Mungu wa kweli mmoja mwenye uwezo wote, muumbajiwa vitu vyote vinavyonekana na visivyoonekana, ambaye binadamu kwa asili yake, hutambua uwezo wake ingawa anaweza kuwa hamjui kwa jina na wapi anaweza kukutana nae. Watu kama haon i wengi katika jamii tunayoishi nayo, ambao Mkristu anapaswa kufundisha wapi pa kumpata Mungu wa Kweli aliyewasilishwa na Yesu Kristu katika Injili, Mungu aliye Upendo, aliyemtoa mwanae Yesu Kristu , awe dhabifu kwa ajili ya kuwakomboa wale wote waaaminio. Na ndivyo kwa kila mbatizwa wa Kanisa, hurithishwa upendo huu wa kutumikia wote kwa upendo kwa manufaa ya jamii. Na kutoka kwa mfano wa maisha yao ya ukarimu na huruma , huuonyesha upendo huu wa Mungu usiokuwa na mipaka.

Mtaguso Mkuu unaonya, ili mafundisho hayo yajizifikie nyanza mbambali za utendaji wa kibinadamu zilizo katika namna nyingi watu bianfsi, familia na maisha ya kijamii , kanisa halina budi, kuambatana na hazina tukufu za ukweli lilioupokea kutoka kwa Mababa wa kanisa bila kuacha. Na wakati huo huo halina bundi kuziangalia ishara za nyakati zilizopo katika mazingira na mienenendo ya maisha , iliyoingizwa katika ulimwengu wa leo , Utume Katoliki ukilazimika kujifunua upya katika hali hizo bila ya kupoteza imani na utambulisho wake.



Baba Mtakatifu Fransisko , katika moja ya homilia zake hivi karibuni alisema , Maisha ya Kikristu hayaishii tu katika kujitafutia imani yake binafsi , bali hutumwa na Kristu kwenda hadi miisho ya dunia kutangaza habari njema ya wokovu, kama Kristu alivyo tii amri ya Baba yake , kuwa daraja la upatanisho, kati ya Mungu na binadamu. Na hivyo Mafundisho ya Kristu , yanamsukuma Mkristu kupeleka ujumbe wa Injili kwa watu wote , kama urithi wao waliokabidhiwa na Kristu mwenyewe. Upendo wa Kristu unawawajibisha kutangaza ujumbe wa amani na upatanisho miongoni mwa watu wote.

Pia Papa Fransisiko katika Katekesi yake juu ya maisha ya sala na tafakari zilizolenga ubatizo, uinjlishaji na ujirani mwema, alimewataka Wakristu wasionee aibu Injili, kwa kuwa hawako chini ya sheria bali chini ya Neema .

Kwa maneno hayo ya Mtakatifu Paulo kwa Warumi, ametaja maana ya kuishi katika neema na uhusiano wake na uinjilishaji kwamba , Neema ni furaha ya kuwa mfuasi wa Kristu , kwa uhuru kamili unaompa heshima ya kuwa mwana wa Mungu. Ni mageuzi yanayo badilisha moyo wa dhambi katika utakatifu. Neema hiyo hutolewa bure na hivyo ni lazima kwa anayeipokea pia kuitoa bure kwa wengine kwa moyo wa ukarimu na shukurani..

Hivyo neema hii inapaswa kuonyeshwa kimaisha na Mkristu katika maisha ya jamii mchanganyiko ambamo kuna waamini na wanaoendelea kutafuta Ukweli na walipoteza matumaini na wasioamini kabisa. Katika haya ya hali mchanganyiko, Papa alimehimiiza waamini kuwa thabiti kiimani, kwa namna gani , ni kupitia kielelezo cha maisha ya furaha kila siku, maisha ya kukubali kupokea mahangaiko ya dunia kama sehemu ya maisha na kukataa yale ya kilimwengu, yanayo elekeza katika utendaji wa dhambi. Ni ushuhuda unaohitaji ujasiri na uvumilivu, kama tabia mbili za Wakristu.

Papa Fransisiko, ametoa mwaliko kwa Wakristu, kujenga ujasiri na uvumilivu huo , wakianza na wao wenyewe, kuwa watu wa kujiamini katika kile wanacho kishuhudia, ndipo waende kwa watu wengine wake kwa waume, kuitangaza huruma ya Mungu na upendo wa Yesu , kuitangaza neema waliyopewa na Kristu.

Aidha Papa ametahadharisha wale wanaodhoofisha juhudi za uinjilishaji kwa kukubikwa na woga na aibu na kukata tamaa, akisema, kukubali hali hiyo, ni kumwalika shetani moyoni. Hakuna sababu za kuogopa kwa sababu silaha ya mapambano haya ni upendo, upendo wa Mungu , Baba Yestu. Ni kuwapenda hata wale wanaotuchukia .

Papa alikiri , kumpenda adui pengine hutufanya tuonekane wanyonge na dhaifu katika kujitetea na pia ni kama kudharirisha heshima na utu wetu, tukionekana kama wapumbavu na maskini, asiyekuwa na maana katika jamii. Lakini katika umaskini ndimo mna mbegu ya ustawi na upendo kwa wengine. Kwa umasikni, Yesu ulileta neema ya wokovu kwa binadamu wote. Na kwa namna gani tunaweza kufanikiwa kuwapenda wote hata maaduni zetu? Ni katika kuwaombea kama Yesu alivyofundisha , salini na waombeeni maaduni zenu na wale wanaowaudhi.

Mama Kanisa katika utume huu wa Uinjilishaji , anasonga mbele zaidi hata katika kazi za binadamu, hasa katika maendeleo ya ajabu ya uvumbuzi unaofanywa na akili za binadamu . Kanisa huingilia kati kwa namna moja au nyingine , kupitia waamini wake kuhakikisha maendeleo hayo yanafanyika kwa misingi ya Injili katika kutunza haki na ukweli wa maumbile. Kwa namna hiyo , huwaonya watu , ili pamoja na jitihada zao katika uvumbuzi mpya, pia wasikose kuyaelekeza macho na nia zao katika utukufu wa Mungu , aliye juu ya vyote vinavyoonekana na visivyo onekana , Mungu aliye asili ya hekima na uzuri wote . Na wasisahau amri inayosema: Msujudie Bwana Mungu wako , Umwabudu Yeye peke yake (Mt 4: 10).

Na hivyo katika nyakati hizi zetu, ambamo dunia imekuwa sawa na kijiji kimoja, bidii zaidi zinahitajika kutoka wa walei zikidai utume uliokomaa zaidi katika kazi za kuijilisha , ili kwenda sambamba na mpanuko wa ongezeko la idadi ya watu, hatua za kazi za maendeleo ya kisayansi na nguvu za teknolijia , pia ujenzi wa mahusiano bora majirani na zaidi kati ya watu katika mchanganyiko wao unaofanikishwa na mfumo wa utandawazi .

Baba Mtakatifu Benedikto XV1, ameasa katika moja ya mafundisho yake kwamba , hakuna sababu za kuongopa Utandawazi. Utandawazi , kama ilivyo katika kukua kwa wimbi la wahamiaji na wakimbizi , unakuwa ni uwanja wa mzuri katika juhudi mpya za Uinjilishaji miongoni mwa jamii yenye imani mchanganyiko . Kwa walei inakuwa ni hitaji linalodai bidii zaidi na hamasa zaidi .

Ishara wazi ya hitaji hilo muhimu , ni kazi ya Roho Mtakatifu , mwenye kutoa ufahamu zaidi na zaidi kwa wanao jihusisha na wajibu huu wa kuieneza Injili, kama wanavyonekana ssehemu zote za dunia, wakikubali mwaliko wa kuwa watumishi wa Kristu na Kanisa lake.

Katika maadhimisho ya mwaka wa imani , hivyo pamoja na mambo mengine ni wakati wa kuizamisha imani yetu kwa Kristu si ndani ya mioyo yetu tu lakini pia kujitahidi kumfikisha Kristu kwa watu wengine. Mafundisho ya Kanisa yanasema, Kanisa Katoliki halikatai yoyote yaliyo ya kweli na matakatifu katika dini zingine. Huheshimu kwa sifa kamili namna za kuishi na kutenda, ingawa zinaweza kuwa tofauti na Kanisa lenyewe, linaamini na kufundisha juu ya nuru ya ukweli wenye kuangaza kwa kila mtu kwamba ni Kristu, ndiye mlango wa uzima wa Milele. Kanisa litaendelea kutangaza hivyo bila ukomo , Kristu ndiye njia ya ukweli na uzima YN14:6. Na ambaye ndani yake wanadamu huuona utimilifu wa maisha ya utauwa na ambamo Mungu alivipatanisha vitu vyote na nafsi yake.

Kwa hiyo Kanisa linawahimiza wafuasi wake , wawe na busara na upendo mwingi kupitia njia ya majadiliano na mazungumzano kujenga ushirikiano wa karibu na wafuasi wa dini zingine kwa amani na maridhiano ili wafuasi wa dini zingine bila ya kushurutisha wauone ukweli wa Injili ya Kristu na kuiongekea.

Katika mwaka huu wa Imani, wafuasi wa Kanisa tunatiwa shime, kuwa mashuhuda wa Injili hasa kupitia mienendo ya maisha yetu ya kila siku, tuonekana kweli watu walio kombolewa na Kristu.
.
Baba Mtakatifu Fransisko kwa maneno ya Mtume Paulo , anahimiza , hatupaswi kuifungia imani ndani ya mioyo yetu bali tunapaswa kuipeleka kwa watu wengine. Tumepewa bure nasi tunapaswa kuitoa bure.
Imeandikwa nami TJ Mhella.








All the contents on this site are copyrighted ©.