2013-06-29 08:57:26

Mshikamano wa upendo na watoto wagonjwa wanaolazwa kwenye Hospitali ya Bambino Gesù mjini Roma


Katika Maadhimisho ya Siku kuu ya Watakatifu Petro na Paulo miamba wa Imani na wasimamizi wa Mji wa Roma, Jumamosi, tarehe 29 Juni 2013, majira ya jioni kunafanyika maonesho maalum ambayo kwa Mwaka 2013 yanatolewa kwa ajili ya heshima ya Baba Mtakatifu Francisko kwa kuchaguliwa kwake kuliongoza Kanisa Katoliki kama Khalifa wa Mtakatifu Petro.

Lengo ni kukusanya fedha zitakazosaidia kununua vifaa maalum kwa ajili ya kitengo cha watoto wanaotibiwa kwenye Hospitali ya Bambino Gesù, inayomilikiwa na kuendeshwa na Vatican. Itakumbukwa kwamba, Hospitali hii imekuwa pia ni msaada mkubwa kwa watoto wanaotoka katika nchi changa duniani. Hospitali ya Mtakatifu Gaspar, Itigi, iliyoko, Manyoni, Singida, Tanzania, imekuwa na uhusiano wa karibu zaidi na Hospitali hii kwa ajili ya huduma kwa watoto wenye magonjwa ya moyo.







All the contents on this site are copyrighted ©.