2013-06-28 12:12:51

Monsinyo Nunzio Scarano amesimamishwa kazi kwa uchunguzi!


Padre Federico Lombardi msemaji mkuu wa Vatican anasema, Vatican inasubiri taarifa rasmi kuhusu kukamatwa kwa Monsinyo Nunzio Scarano anayetuhumiwa kujihusisha na mchakato wa utakatishaji wa fedha chafu. Kwa takribani mwezi mmoja uliopita, Nunzio Scarano ambaye alikuwa anafanya kazi katika Idara ya fedha (APSA) mjini Vatican alisimamishwa kazi kwa uchunguzi.

Vatican imeonesha utayari wa kushirikiana na Serikali ya Italia ili kupata ukweli wa tukio hili. Wakati huo huo, Vatican AIF inaendelea kuchunguza tukio hili kama itabidi kuchukua hatua stahiki!







All the contents on this site are copyrighted ©.