2013-06-27 10:21:46

Papa Francisko ni kati ya viongozi mashuhuri wanaoendelea kuitikisa dunia kwa sasa!


Utafiti uliofanywa na Shirika la Habari la Adnkronos na kuchapishwa katika kitabu chenye kurasa 960, unaonesha kwamba, Baba Mtakatifu Francisko ni kati ya watu mashuhuri walioitikisa dunia katika kipindi cha Mwaka 2013. Kitabu hiki ambacho kiko tayari mitaani, kina ujumbe muhimu uliotolewa na Baba Mtakatifu Francisko kwa wakuu wa Serikali na Jumuiya ya Kimataifa katika medani mbali mbali za maisha pamoja na watu wenye mapenzi mema.

Baba Mtakatifu anawataka viongozi hao kuhakikisha kuwa, wanatunza mazingira, kielelezo cha mpango wa Mungu ulioandikwa katika mazingira na kwamba, wanapaswa kuwa ni walinzi kwa jirani zao. Hii ni changamoto ya kujikita katika maendeleo endelevu!







All the contents on this site are copyrighted ©.