2013-06-25 15:03:58

Padre Murad auwawa kinyama nchini Syria


Kardinali Leonardi Sandri, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki anaungana na viongozi wakuu na waamini wa Makanisa ya Mashariki kuomboleza kifo cha Padre Francois Murad, aliyeuwawa kikatili siku ya Jumatatu, tarehe 24 Juni 2013 nchini Syria.

Marehemu Padre Murad amekumbukwa katika sala pamoja na marehemu wote waliokwisha poteza maisha yao kutokana na vita inayoendelea nchini Syria kwenye Kikanisa cha Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki.

Ukatili wa namna hii hauwezi kukubalika, kuna haja kwa wakuu wa Jumuiya ya Kimataifa kusimama kidete ili hatimaye, kuibua mbinu mkakati utakaosaidia kusitisha vita hii, ili hatimaye, kuanza mchakato wa upatanisho, haki na amani. Ni matumaini ya Wakristo nchini Syria kwamba, wataendelea kubaki na kushiriki katika utangazaji wa Habari Njema ya Wokovu kwa kuonesha ile sura ya Kristo.







All the contents on this site are copyrighted ©.