2013-06-24 11:02:08

Watoto wakutana na Papa Francisko!


Baraza la Kipapa la Utamaduni kwa kushirikiana na wadau mbali mbali, Jumapili tarehe 23 Juni 2013 waliaandaa Treni maalum kwa ajili ya watoto wenye umri kati ya miaka sita hadi kumi waliosafiri kutoka Kaskazini mwa Italia hadi Roma na kupokelewa na Baba Mtakatifu Francis aliyewashukuru kwa kufika mjini Vatican.

Baba Mtakatifu amezungumza na watoto hao kwa njia ya maswali na majibu. Waandaaji hao wamemshukuru Baba Mtakatifu kwa kuwaonjesha upendo na ukarimu. Watoto wamepata bahati ya kutembelea Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican.







All the contents on this site are copyrighted ©.