2013-06-24 15:16:28

Papa akutana na watetezi wa haki msingi za binadamu kutoka Argentina


Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu, tarehe 24 Juni 2013 amekutana na kuzungumza na Bwana Adolfo Pèrez Esquivel, Mshindi wa Tuzo ya Amani mjini Vatican, aliyekuwa ameambatana na Bwana Felix Diaz, mkuu wa Kabila la Qom lililoko nchini Argentina pamoja na ujumbe wao!

Viongozi hao wamemshukuru na kumpongeza Baba Mtakatifu kwa kuwapatia fursa ya kuzungumza nao pamoja na jitihada zake za kuwalinda na kuwatetea wazawa wa Argentina na Amerika ya Kusini katika ujumla wake. Viongozi hao wanasema, wanaguswa sana na uvunjifu wa haki msingi za binadamu wanazofanyiwa wazawa wa Argentina na Amerika ya Kusini katika ujumla wao hasa kuhusiana na utambulizo na ardhi yao!

Taarifa hii imetolewa na Padre Federico Lombardi, msemaji mkuu wa Vatican.







All the contents on this site are copyrighted ©.