Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini, Jumatatu, tarehe 24 Juni 2013 amewaambia waandishi
wa habari kwamba, hali ya Mzee Nelson Mandela inaendelea kudhohofu na kwamba, bado
amelazwa Hospitalini na madaktari wanaendelea kumhudumia kadiri ya uwezo wao. Nayo
Familia ya Mzee Madiba inawaomba wananchi wa Afrika ya Kusini kuendelea kumwombea
Mzee Madiba katika sala na dua zao. Wao kama familia wametulia na wanafuatilia taarifa
za madaktari.