2013-06-22 10:45:01

Watawa wanahimizwa kushirikiana na kushikamana kwa ajili ya kumhudumia Mungu na jirani!


Shirikisho la Mashirika ya Kitawa na Kazi za Kitume Afrika na Madagascar, COSMAM, hivi karibuni limehitimisha mkutano wake uliofanyika huko Libreville, nchini Gabon. Lengo la mkutano wa wakuu wa Mashirika ya Kitawa na Kazi za Kitume lilikuwa ni kuyajengea uwezo Mabaraza ya Wakuu wa Mashirika ya Kitawa na Kazi za Kitume, Afrika ya Kati, ili kujenga na kuimarisha madaraja ya uhusiano wao na Kristo Yesu anayewaita kujitoa bila ya kujibakiza kwa ajili ya huduma kwa Mungu na jirani zao ndani ya Kanisa Katoliki.

Shirikisho hili ambalo linaunganisha Mashirika mbali mbali ya Kitawa na Kazi za Kitume linamepewa jukumu na Mama Kanisa la kuhakikisha kwamba, linayasaidia Mabaraza ya Mashirika kutekeleza wajibu na utume wao wa Kimissionari, ili kujenga na kuimarisha umoja na mshikamano wa kitume sanjari na kuwawezesha watawa kuishi kikamilifu wito wao kwa kushirikiana na Mashirika mengine kwa ajili ya sifa na utukufu wa Mungu na maendeleo ya binadamu.







All the contents on this site are copyrighted ©.