Ninyi ni Wachungaji mliombeba Kristu ndani mwenu- Papa.
Ninyi ni wajumbe wa kumpeleka Kristu ulimwenguni. Na kamwe msisahau kwamba ninyi
ni wachungaji, mnao mwasilisha Kristu ulimwenguni, mkiwa watu mlio achana na roho
wa kipebari na maisha ya kidunia ambamo mna hatari ya kukebehi hata utume Mtakatifu
wa kuwa mwakilishi wa Papa .
Papa Fransisko , alitoa ujumbe huo kwa Mamia
ya wawakilishi wa Papa ambao pia wanajulikana kwa jina la Wajumbe wa Kitume au Manusio,
ambao katika ujumla wao wote wamekusanyika Vatican toka pande zote za dunia, kwa ajili
ya mkutano kisala na tafakari kwa muda wa siku mbili, katika mtazamo wa Mwaka ya
Imani.
Akiwahutubia siku ya Ijumaa, Baba Mtakatifu Fransisko, aliangalisha
katika Mwaka wa Imani . Na mwanzo alitoa shukurani zake za dhati kwa Bwana kwa majaliwa
yake ya kuwakusanya pamoja na katika muda huu w siku mbili wa tafakari na sala, wakiwa
wmashikamana pamoja katika hali ya udugu na umoja chini ya Kiti cha Petro na Askofu
wa Roma. . Na aliwashkuru wote kwa maneno mazuri yaliyotolewa na Kardinali Bertone,
kwa niaba yao wote, na kwa huduma yao nzuri, wanayo itoa kwa niaba yake na kwa niaba
ya kanisa zima katika utume wa umoja na Khalifa Mtume Petro,akisema, na hivyo ni
wawakilishi wake katika makanisa yaliyotwanyika duniani kote na kwa serikali na katika
maana ya kutoa sura ukatoliki wa Kanisa la ulimwengu .
Papa , ameonyesha
kutambua kwamba, maisha ya Nunsio , ni maisha ya kuhamahama , toka sehemu moja hadi
nyingine, bara hadi bara, taifa hadi taifa na ndivyo wanavyobadilisha hali halisi
za maisha ya kikanisa, na aliwashukuru kwa kukubaliana na hilo na kuweza kuyaishi
maisha hayo. Papa ameyataja maisha hayo, kwmba huotoa picha msafiri, katika mtazamo
wa kina wa maisha ya imani, kama ilivyokuwa kwa Ibrahimu, mtu wa imani katika safari:
Mungu alimtaka aondoke nchi yake, na kuayaachamazingira aliyoyazoea na kuanza mwendo
kwa kuamini ahadi ya Mungu . Na aliendelea kuwa namtu wa imani na tumaini , kama
ilivyoandikwa kaitak kitabu cha Mwanzo.
Papa alieleza na kutaja kwamba kuna
orodha ya mifano ya mingi ya Mababa wa Imani walioiingigia safari hii ya imani na
kuona matokeo ya ahadi ya Mungu. Maisha kama hayo yana thamani kubwa , na ni maisha
kama yao , pale wanapo yaishi kwa upendo mkuu na wa kina na kwa kumbukumbu za wito
wao wa kwanza .
Pia aliendelea kutafakari juu ya kuona mbali , akiitazama
tena mifano mingi iliyoandikwa katika Agano la Kale na kuwahimiza Mabalozi wa Papa
kuwa na mtazamo huo kama msingi wa msukumo wa ndani, wa unao toa nguvu za kusonga
mbele kumtafuta Kristu, , ambaye ndiye ahadi yetu.
Na aliwarejesha katika
barua maarufu ya Aprili 25, 1951, hotuba ya aliyekuwa Katibu Mbadala wa Nchi kwa
wakati huo, , Monsignor Montini, iliyomzungumzia maana ya kuwa mwakilishi wa Papa,
kwamba, ni yule mwenye kuwa na ufahamu wa kweli kwamba, ndani mwake yu pamoja na
Kristu kama hazina ya thamani anayotakiwa kuiwasilisha kwa watu. Kujenga mahusiano
ya karibu na Yesu Kristo lazima iwe kula chakula cha Krsitu kila siku, kwa sababu
ni katika chakula hicho, ndicho kinawarejesha daima, katika kumbukumbu ya kwanza
ya kukutana na Kristu, na pia kwa sababu ni kielelezo za uaminifu cha kila siku
katika wito wao. Kuwa karibu na Kristu katika sala , maadhimisho ya Ekaristi, katika
huduma ya upendo.
Papa pia aliwaasa Mabalozi juu ya hatari YA kusalimisha
wito wao kwa roho wa kupenda dunia: kujisalimisha katika roho wa malimwengu, ambayo
hatua kwa hatua huongoza katika ubinafsi , kiburi na majivuno. Huko humwondoa mtu
katika kuwa mtumishi kwa ajili ya utukufu wa Mungu. Papa aliwaasa juu ya aina ya
"roho huyo wa ubepari na maisha ya starehe ambayo hatima yake huwa ni majuto. Na
pia alionya juu ya roho huyo wa kidunia anayejificha ndani , hata wakati mwingine
hujenga roho wa kejeli ,unafiki na usaliti , kwa wanaonekana kukubaliana na wengine
lakini kumbe kuna tabia ya kukosoa wengine nyuma ya migongo ya wenzao.
Papa
aliwakumbusha Mabalozi hao, wasisahau utume wao wa kwanza ni kuwa ni Wachungaji.
Wao ni wawakilishi wa Papa , wawakilishi wa upendo wa Kristu, wawakilishi wa kikuhani
kama wachungaji, ingawa si kama maaskofu wa eneo fulani au viongozi wa mtaa fulani
wa Kanisa, lakini ninyi ni Wachungaji wanaotumikia Kanisa, wahamasishaji na wahudumu
wa usharika,kazi ambao si rahisi na yenyekudai majitoleo , na daima yenye kuhitaji
kumulikiwa na upendo wa kina! Hata katika mahusiano na Mamlaka za Kiraia na Wale
wanaowasaidia bado ni ninyi ni wachungaji , wanaotakiwa daima kutafuta mazuri kwa
ajili ya wote , mema ya Kanisa na ya kila mtu, alisisitiza Papa .
Papa alihitimisha
hotuba yake kwa kuwataka Mabalozi hao , kuivaa roho ya upole, uvumilivu na huruma;
wakihamasihswa na umaskini wa ndani na uhuru wa Bwana na pia na kuwa wanyenyekevu
katika wa maisha, bila ya kutafuta makuu, wakijiepusha na tamaa na ubabe wa madaraka.
Wajione kuishi kw aunyenyekevu wa kuwa wachumba wa Kanisa la Kristu.. wakwia wamevalishwa
uwezo wa kulichunga kundi la kondoo waliodhaminishwa kwao. Kulitunza na kudumisha
tumaini la nuru ya wokovu katika mioyo yao, kwa upendo na uvumilivu, na kwa msaada
wa kudra ya Mungu kwa watu wake. Papa alieleza kwa kuwatazamisha katika mfano wa
maisha ya familia Takatifu, jinsi Mt. Yosef, alivyomtunza Maria na Yesu.
Na
aliwakaribisha kuendelea kutafakari juu ya huduma yao muhimu na ya thamani kubwa
kwa Kanisa lote,a ktika mtazamo kwamba, maisha yao ni hija ya kuendelea kutembea bila
ukomo wa kuwa na kituo kimoja cha kutulia kwa muda mrefu sehemu moja, au katika
utamaduni mmoja, au katika hali halisi maalum za kikanisa. Ni maisha kwenye barabara
kutembea daima na Yesu Kristo mwenyewe aliye wabariki kwa mkono wake.