2013-06-21 15:41:10

Weka hazina moyoni na si katika ghala la kidunia- Papa


Kumwomba Mungu Neema ya kuwa na moyo wa kujua kupenda , ni kujiwekea hazina moyoni. Papa Fransisko , alieleza wakati wa Ibada ya Misa mapema Ijumaa asubuhi katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta mjini Vatican.

Ibada aliiongoza akisaidiana na Kardinali Fransisko Coccopalmerio, pamoja na Askofu Juan Ignacio Arrieta na José Aparecido Gonzalves de Almeida, ambao ni rais, katibu na Katibu mwandamizi wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Maandiko ya Kisheria. Walikuwepo pia baadhi ya wafanyakazi wa idara za baraza hilo, na wafanyakazi wa kiwanda binafsi cha Kanisa Kuu la Yohane wa Laterano , wakiongozwa na Msgr. James Ceretto, na wafanyakazi wengine katika jengo la Domus Sanctae Marthae.

Papa alieleza jitihada za kuiwinda hazina hii, ambayo ina nguvu za kutupeleka pia katika maisha ya baadaye, baada ya maisha haya ya kawaida, ambayo ndiyo dhamira ya Mkristo. Daima kuwa na hazina hii, kama Yesu alivyowaambia wafuasi wake, kama iivyoandikwa katika kifungu cha Injili ya Mathayo: "mahali ilipo hazina yako, ndipo pia yalipo mapenzi ya moyo wako.
Papa ameeleza na kubaini hatari iliyopo ya kuchanganya hazina hii na hazina za kidunia zidanganyazo ambazo Mkristu ni lazima kuziambua na kujiweka mbali nazo , ambazo hulindikana wakati wa maisha lakini hutoweka mara baada ya kifo kutokea.

Papa alieleza, na kutoa mfano kwamba , katika maisha yake hajawahi kuona, mali ya marehemu ikiandamana hadi kaburini “Sijawahi kuona lori, mali ya marehemu ikiandamanishwa katika msafara wa maziko ili ikazikwa na marehemu. Lakini utajiri wa kiroho huandamana na mtu hadi kaburini. Hakuna anayeweza kuipokonya toka wka mmliki , hivyo mtu huzikwa nayo na kuendelea kuwa nayo katika maisha ya milele.

Hazina hii ya kiroho, pia tunaweza kuitoa pia kwa watu wengine na kwetu isipungue kitu. Hazina hii inakuwa ni sifa yetu na haki yetu yakuwa na Yesu ndani mwetu. Na hiyo ndiyo tunayotakiwa kuibeba muda wote. Na ndiyo tunatakiwa kuipeleka kwa wengine, nayo ni hazina ya upendo , huduma, uvumilivu, wema na huruma. Ni hazina nzuri ya kuihifadhi moyoni muda wote alisisitiza Papa Fransisko.

Kwa hiyo, kama ilivyoandikwa katika Injili , Papa aliendelea , hazina ya thamani machoni pa Mungu, ambayo tunajikusanyia hapa dunia na pia hukusanywa mbinguni kwa ajili yetu.
Papa alieleza na kuonya juu ya utafutaji wa hazina zinazotuweka mbali na Bwana. Hazina zinazohaingaisha na kuuchosha moyo , kufikiria tu juu ya mali za kidunia zisizorithisha moyo. Wakati kuitafuta hazina ya upendo unaotajwa na Kristu huutuliza moyo na kufarijika hata kimwili.
Katika hatua hii, anasema Papa Francisko , Kristo amelitaja “jicho", ambayo ni ishara ya "nia ya moyoni" na yale yanayo jitokeza kimwili kwamba , moyo wa upendo huangazia nuru mwili, na moyo mbaya, huupeleka mwili gizani. Papa aliomba maombezi ya Mtakatifu Luigi Gonzaga aliyekumbukwa na Kanisa leo, ili Bwana atujalie neema ya moyo mpya,"moyo wa nyama":








All the contents on this site are copyrighted ©.