2013-06-20 09:03:49

Kilio cha amani kwa ajili ya Nchi Takatifu


Kardinali Leonardo Sandri, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki na Rais wa ROACO, Jumanne, katika Ukumbi wa Kanisa la Mtakatifu Maria la Transportina, Roma, aliongoza Mkutano wa Mwaka wa Shirikisho linalounganisha misaada Katoliki kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki (ROACO)

Hotuba ya kufungua Mkutano huo iliyotolewa na Kardinali Sadri ililenga katika mambo manne, kwanza , ukuu wa adhimisho la Fumbo la Ekaristi Takatifu kwamba, muumini hujikuta ndani ya moyo wa Mungu kwa njia ya upendo wa msalaba na ufufuko wa Bwana watu Yesu Kristu , ambamo Roho Mtakatifu hutoka bila kipimo kwa kila anayempokea. Na alitoa mwaliko kwa kila mjumbe wa mkutano huu ,kujifunua, kuwajibika na kujidhaminisha kwa Mungu, na kuelekeza nia nzote kwa ajili ya mazuri kwa watu wote wa Mashariki ya Kati, wakijiruhusu kuongozwa na neema zake Mungu.

Na kwamba, kipaumbele chao kinabaki kuwa kilekile , mshikamano thabiti wa Kikristu, wenye kupata dhamana yake kupitia mawasiliano ya mara kwa mara na Maaskofu na Wachungaji wa Makanisa kijimbo, ambayo hushirikiana na vyombo vya ROACO,pamoja na shughuli za uratibu unaotolewa kwa hiari na Umoja wa ROACO, katika kutoa jibu kwa mamlaka ya Askofu wa Roma, ambalo ni kueneza katika mipaka yote, kwa watu wote wa Mashariki, udugu na kujali wengine.

Kardinali aliendelea kuzama katika fumbo la Ekaristi akisema, daima huwezesha kuamusha ari mpya ya neema inayotuwia kuwa na deni kwa Mungu, Kristo akiwa madhabahu yetu yasiyoweza kuharibiwa. Na ni Yeye Kuhahi Mkuu wa milele. Yeye mteswa asiyekuwa na doa ambaye alifanyika kuwa sadaka yetu wenyewe kamili , ambayo ni pamoja na zawadi ya maisha yetu kwa Mungu katika utii wa imani.

Kwa sababu Kristo hutuunganisha naye Mungu, , na hivyo hutuwezesha na kudumu katika safari ya kuelekea kwenye ukamilifu wa kikristo, hata hivyo, yenye kudai, kwa kuwa ni kipimo kwa upendo kinzani wa Msalaba. wapendeni adui zenu na kuwaombea wale wanaowadhulumu ninyi.

Kardinali pia aliwakumbuka pia wafadhili wa Makanisa ya Mashariki, wotei walio hai na marehemu. Na pia wengi ambao pia wanajiunga katika mateso ya Wakristu wa Mashariki kwa namna moja au nyingine, kwao wote wanastahili shukurani na heshima kubwa kwa kuwa washariki wa kuubeba msalaba huu wa mateso makubwa yanayoendelezwa katika nchi ulikozaliwa Ukristu.

Alitolea sala ili Bwana, awawezeshe Wakristu Mshariki ya Kati, kupata ujasiri, upole, uvumilivu na nguvu za kuyaishi hayo wakiwa wamejawa na faraja ya imani, pamoja na wale wanaoshiriki katika hatima yao ya kutisha. Na ili kamwe wasishikwe na harahara za kutaka kutoa jibu la chuki kwa chuki; au kulipa kisasi , au kushakia uwezo neema ya Mungu, katika hatima ya kuvunja uovu mwingi.

Na mwisho aligeukia uwepo wa "Wakuu na Mababa" ya Makanisa Kikoptic na Kikaldayo, na Wajumbe wa Kitume na Wajumbe wengine, akisema , wote kwa pamoja wamejumuika kama kundi moja , kutolea kilio chao kwa ajili ya amani Mashariki ya kati. Na wakiwa na lengo moja la kuwakumbatia katika Bwana, waamini wote wa Makanisa ya Mashariki, waliomo ndani ya Mashariki ya kati na hata sehemu mbalimbali za dunia, kama matokeo, ya hofu za kuteseka na waliopoteza makazi yao ya asili, hasa mizizi yao ya kiroho.

Katika mtazamo huo na kwa maombezi ya Mama Maria Mtakatifu Sana mfano wa ukarimu wa kimama , na awadumishe wote katiak moyo wa upeondo na ukarimu usio na mashaka kwamba Bwana ndiyemwenye kumweka mtumwa huru na ndiye anayewatangulia katiak safari yamaisha hapa duniani mwenye kumtia nguvu mjane na yatima, lakini njia ya waovu huiangamiza. Amina







All the contents on this site are copyrighted ©.