Katika Maadhimisho ya Mwaka wa Imani, Shirika la Posta nchini Italia limetoa zawadi
ya magari madogo mawili kwa Baraza la Kipapa la uhamasishaji wa Uinjilishaji Mpya,
kwa ajili ya matumizi ya Maadhimisho ya Mwaka wa Imani. Haya ni magari ambayo hutumiwa
na wafanyakazi wa Posta kwa ajili ya kusambaza barua nchini Italia.
Askofu
mkuu Rino Fisichella, Rais wa Baraza la Kipapa la uhamasishaji wa Uinjilishaji Mpya
amelishukuru Shirika la Posta Italiani kwa mchango wake katika Maadhimisho ya Mwaka
wa Imani, unaotarajiwa kufungwa rasmi, Mwezi Novemba, 2013.