2013-06-18 09:30:30

Papa akutana na Rais wa Venezuela


Jumatatu Papa alikutana na Rais wa Venezuela , Mheshmiwa Nicolas Maduro. Mkutano wao ulilega zaidi masuala ya kijamii na kisiasa kulingana na hali halisi za taifa hilo, hasa baada ya kifo cha Rais aliyependwa sana na watu Hugo Chàvez, na pia juhdi za kutokomeza ufukara na mapambano dhidi ya uhalifu na biashara haramu ya dawa za kulevya .
Wakuu pia walijadili, uwepo wa historia ya kanisa katika taifa la Venezuela, na juhudi zake katika kuchagia utoaji wa elimu, huduma za afya na matendo mengine ya huruma. Na waliona kuna haja ya kuwa na majadiliano ya kweli na thabiti mara kwa mara kati ya Baraza la Maaskofu la Venezuela na serikali , kwa ajili ya ufanikishaji haraka zaidi, maendeleo katika taifa lote. Na mwisho walilenga katika hali za kimkoa katika mtazamo maalum wa amani kwa taifa lote la Venezuela.
Mwisho wa mkutano wao , Papa na Rais Maduro waliibadilishana zawadi.








All the contents on this site are copyrighted ©.