Kutetea maisha ya binadamu si tu haki na wajibu kwa Wakristu, lakini ni wajibu kwa
watu wote, Askofu Mkuu Fischella.
Jumapili wakati wa kukamilisha Ibada ya Misa katika Kanisa Kuu la Mtaktifu Petro,
Askofu Mkuu Rino Fischella, Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Kukuza Uinjilishaji
Mpya , alitoa salam zake kwa Baba Mtakatifu Fransisko, kwa ajili ya adhimisho hili
la Siku ya Injili ya Maisha. . Katika salaam hizo , kwanza aliutambulisha Umati
wa waaamini waliohudhuria Ibada ya Misa akisema, wingi wa watu hawa waliotoka pande
mbalimbali za duniani , ni ushuhuda dhahiri kama Injili ya Yohana inavyosema, maisha
yamedhihirishwa. Katika salaam hizi, Askofu Mkuu Fisichella, alionyesha shukurani
za dhati kwa Papa kwa msaada wake na nguvu za ushahidi wake, katika kuyatetea
na kuyalinda maisha. Katika maadhimisho ya Ibada ya Misa siku ya Jumamosi asubuhi,
umati mkubwa wa wawakilishi wa vyombo vya kutetea maisha , wake kwa waume walihudhuria
ibada hiyo kwa ajili ya maadhiisho Siku ya Injili ya Maisha, ikiwa ni alama ya neema
kuguuguswa na mwili wa Kristo na hivyo kuwa watetezi imara wa hadhi ya maisha. Askofu
Mkuu Fischella, aliutaja umati huo, kuwa ni mashahidi wa upendo, ambao kamwe haukosi
kuwa karibu na watoto na walio telekezwa, wenye kusumbuliwa na maradhi sugu, walemavu,
watu walio katika hali za kufa na waliotupwa pembezoni na jamii, kwa tamaa za dhambi
na ubinafsi wa mtu. Na aliogeza katika Mwaka wa Imani, inakuwa ni wakati muhimu
wa kutafakati na kusali kwa ajili ya wale wanao yatolea maisha yao kama mashahidi
wa Injili ya Maisha. Shauku ya maisha yao ya kila siku inaonyesha wazi dhamira ya
kukuza kikamilifu zawadi ya maisha ya binadamu na kwa ajili ya utetezi wake. Kufanywa
upya katika wito kwa kila mtu na kuheshimu, kulinda, kupenda na kumtumikia maisha
ya binadamu, si tu haki na wajibu wa Wakristo, lakini ni maisha ya kawaida kwa
watu wote , wanaume kwa wanawake, hata ambao si Wakristu.