Rais Jakaya Mrisho Kikwete amealikwa kuiwakilisha Tanzania na Afrika katika shughuli
za Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Nchi Zenye Viwanda Vingi Duniani – G8 wa mwaka huu
unaofanyika London, Uingereza. Rais Kikwete ambaye pia alihudhuria mkutano wa mwaka
jana wa G-8 Marekani kwa mwaliko wa Rais Barack Obama, amealikwa na Waziri Mkuu wa
Uingereza, Bwana David Cameron kuhudhuria mkutano wa mwaka huu.
Rais Kikwete
ambaye atashiriki katika kikao cha kujadili ukuaji wa uchumi ataungana na Rais John
Mahama wa Ghana, Rais Alpha Conte wa Guinea, Rais Hassan Sheikh Mahmound wa Somalia
na Rais Blaise Compaor’e wa Burkina Faso kushiriki katika kikao hicho. Rais Kikwete
ameandamana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka
na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.