2013-06-15 14:30:09

Kongamano la Kikanisa Jimbo kuu la Roma kuanza kutimua vumbi, Jumatatu tarehe 17 Juni 2013 kwa Katekesi ya Papa Francisko!


Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu jioni tarehe 17 Juni 2013 anatarajiwa kufungua Kongamano la Jimbo kuu la Roma, ambalo kwa mara ya kwanza litafanyika mjini Vatican kuanzia saa 1:30 Jioni kwa saa za Ulaya. Baba Mtakatifu anatarajiwa kutoa Katekesi inayoongozwa na kauli mbiu "Mimi sioni aibu kwa Injili". Mada ya Kongamano hili ni umuhimu wa Yesu katika maisha ya waamini. Waamini wanatambua kwamba, wanao wajibu wa kutangaza Habari Njema ya Wokovu hadi miisho ya dunia.

Viongozi mbali mbali wa Kanisa kutoka Jimbo kuu la Roma watashiriki katika Kongamano hili. Jumanne tarehe 18 Juni 2013, Kongamano litahamishiwa kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Yohane wa Laterano. Hii itakuwa ni fursa pia kwa Jimbo kuu la Roma kuonesha mwelekeo wa mikakati na shughuli za kichungaji Jimboni humo. Kongamano linahitimishwa, Jumatano tarehe 19 Juni 2013.







All the contents on this site are copyrighted ©.