2013-06-15 14:18:31

Bwana Josè Barroso akutana na kuzungumza na Papa Francisko!


Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi tarehe 15 Juni 2013 amekutana na kuzungumza na Bwana Josè Manuel Durao Barroso, Rais wa Tume ya Ulaya, ambaye pia alikutana na Kardinali Tarcisio Bertone, Katibu mkuu wa Vatican pamoja na Askofu mkuu Dominique Mamberti, Katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican.

Baba Mtakatifu na mgeni wake wamejadili kuhusu masuala ya kimataifa na kikanda; myumbo wa uchumi kimataifa na athari zake katika maisha ya vijana na familia. Wamegusia pia mchango wa Kanisa katika ustawi na maendeleo ya wananchi wa Ulaya kiroho na kiutu.

Wamekazia umuhimu wa kusimama kidete kulinda na kutetea haki msingi za binadamu hususan uhuru wa kidini pamoja na kukomesha madhulumu ya Wakristo sehemu mbali mbali za dunia.







All the contents on this site are copyrighted ©.