2013-06-12 14:47:51

Mh. Padre Luiz Fernando Lisboa ateuliwa na Papa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Pemba, Msumbiji


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Luiz Fernando Lisboa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Pemba, nchini Msumbiji. Askofu mteule alizaliwa tarehe 23 Desemba 1955 mjini Rio de Janeiro, Brazil. Baada ya majiundo yake ya kitawa kwenye Shirika la Mapadre wa Mateso, tarehe 23 Januari 1977 aliweka nadhiri zake za mwanzo na tarehe 18 Desemba 1982 akaweka nadhiri za daima.

Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, akapadrishwa tarehe 10 Desemba 1983. Katika maisha na utume wake kama Padre na mtawa amejishughulisha zaidi na masuala ya kichungaji Parokiani; malezi seminarini. Kuanzia mwaka 2001 hadi mwaka 2010 alitekeleza utume wake kama Paroko, Jimbo Katoliki la Pemba, Msumbiji na mkufunzi wa masuala ya kitaalimungu kwa waamini walei. Baadaye alirejea nchini Brazil kwa mapumziko mafupi.







All the contents on this site are copyrighted ©.